Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Eden Hazard ana ndoto za kurudi Chelsea

576912938eda8a3cd6892ebe26d1598c Crop North 660x400 Eden Hazard ana ndoto za kurudi Chelsea

Wed, 22 Jul 2020 Chanzo: millardayo.com

Mshambuliaji wa pembeni wa Mabingwa wa Hispania Real Madrid, Eden Hazard amesema huenda akarejea jijini London kujiunga na waajiri wake wa zamani Chelsea, kutokana na kukoshwa na aina ya wachezaji wapya ambao wapo njiani kusajiliwa majira ya kiangazi.

Hazard amesema anafikiria kurudi hapo siku moja na mashabiki wa Chelsea wategemee hilo, kwa kuwa mastaa kama Timo Werner na Hakim Ziyech wanampa mzuka wa kutaka kucheza nao.

Chelsea tayari imejihakikishia kuziapata saini za Hakim Ziyech kutoka Juventus na Timo Werner kutoka RB Leipzig, Pia wapo kwenye mpango wa kuhakikisha wanaipata saini ya Kai Havertz wa Bayer Leverkusen ambaye ripoti zinadai wameongeza juhudi za kuhakikisha wanaipata saini yake.

“Nitarudi ikiwa nitamaliza kilichonileta hapa, huwa naangalia mechi zao japo sio mara nyingi, kiukweli wanafanya vizuri, kuna vijana wengi kwenye timu ambao wana viwango vizuri, kwa sasa wanaweza kununua wachezaji kwa bei kubwa kiukweli nafikiri siku moja nitarudi hapo” Hazard

MWANA FA ALIVYOOMBA KURA MUHEZA “NIMESOMA UINGEREZA, MSOMI MZURI, NAUMIA SANA”

Chanzo: millardayo.com