Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

EXCLUSIVE: Simon Msuva baada ya kufunga hat-trick yake ya kwanza kimaifa

3135 Screen Shot 2018 02 12 At 6.03.43 PM 660x400.png

Tue, 13 Feb 2018 Chanzo: millardayo.com

Mtanzania Simon Msuva anayecheza soka la kulipwa katika club ya Difaa El Jadida ya Morocco Jumamosi ya Febeuary 10 2018 ameichezea timu yake ya El Jadida game yake ya kwanza ya club Bingwa Afrika dhidi ya Sport Bissau E Benfica ya Guinea Bissau.

Msuva alikuwa sehemu ya kikosi cha Difaa El Jadida kilichocheza dhidi ya Sport Bissau E Benfica na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli 10-0, kwa upande wa Msuva amefanikiwa kufunga hat-trick katika game hiyo na kuhusika katika upatikanaji wa magoli matatu mengine akitoa pasi mbili za magoli na akisababisha penati.

AyoTV imeongea na Simon Msuva kutokea Morocco “Weekend hii tumecheza mechi na timu ambayo inatoka Guinea, nashukuru Mungu mechi yetu tulimaliza salama na tulishinda magoli 10-0 katika ushindi huo nilitoa pasi mbili za goli na kusababisha penati iliyozaa goli, kwa upande wangu ni hat-trick yangu ya kwanza kimataifa sikuwahi kufunga kimataifa”>>>Msuva

VIDEO:Magoli ya Simba walivyorudi kimataifa leo vs Gendermarie Full Time 4-0

Chanzo: millardayo.com