Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dube na kibarua cha kumvua ufalme Kagere, VPL

PRINCE Dube na kibarua cha kumvua ufalme Kagere, VPL

Sat, 22 May 2021 Chanzo: eatv.tv

Mshambuliaji wa Azam FC Prince Dube ameendeleza moto wake wa kupachika mabao kwenye michezo ya ligi kuu soka Tanzania bara, sasa amefikisha mabao 14 akiwa ndio kinara wa ufungaji msimu huu akiongoza kwa tofauti ya mabao matatu dhidi ya Meddie Kagere wa Simba mwenye mabao 11.

Dube alifunga bao lake la kumi na nne msimu huu jana usiku kwenye mchezo wa Ligi dhidi ya Biashara United, mchezo uliochezwa katika dimba la Azam Complex na Azam iliibuka na ushindi wa mabao 2-0, Dube alifunga bao la kwa dakika ya 11 na bao la pili lilifungwa na Mudathir Yahya dakika ya 54.

Mshambuliaji huyo raia wa Zimbabwe huu ni msimu wake wa kwanza akicheza Ligi Kuu soka Tanzania bara, alijiunga na Azam mwanzoni mwa msimu huu kwa mkataba wa miaka miwili (2) akitokea Highlanders FC ya Zimbabwe.

Dube mwenye umri wa miaka 23, huwenda akauzima ufalme wa Meddie Kagere wa Simba ambaye ametwaa tuzo ya ufungaji bora wa VPL kwenye misimu miwili iliyopita, ambapo msimu wake wa kwanza Kagere alifunga mabao 23 na msimu ulipita alifunga mabao 22 na msimu huu raia huyo wa Rwanda ameshafunga mabao 11 akiwa nafasi ya pili.

Kwenye mbio hizo za kuwania kiatu za mfungaji bora, Azam FC ya Prince Dube imebakiza michezo minne kabla ya kumaliza msimu wakati Simba ya Kagere bado inamichezo tisa kabla ya kumaliza msimu.

Kwenye orodha ya ufungaji ukimtoa Dube na Kagere wanaoshika nafasi ya kwanza na ya pili, wachezaji wengine wanaofata ni John Bocco wa Simba ana mabao 10, Ibrahim Meshack wa Gwambina ana bao 9 na Daniel Lyanga wa JKT Tanzania nae ana bao 9.

Chanzo: eatv.tv