Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Drake ashinda Bilioni 6.28 ushindi wa Adesanya

Rapper Drake Wins 2 Drake ashinda Bilioni 6.28 ushindi wa Adesanya

Sun, 9 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rapa maarufu wa Canada, mwimbaji na mtunzi wa nyimbo Drake ameshinda dola milioni 2.7 (Tsh bilioni 6.28 ) baada ya Bondia Israel Adesanya wa Nigeria kumbwaga Alex Pereira raia wa Brazil kwenye UFC 287 na kutetea tena taji lake la uzito wa kati.

Adesanya alishinda tena taji hilo kwa KO katika raundi ya pili miezi mitano tu baada ya kushindwa na Pereira, ambaye hapo awali alimshinda mara mbili katika mchezo wa ndondi.

Drake alipoteza dola milioni 1.6 baada ya kumwekea dau Adesanya kushinda katika pambano hilo lakini amepindua meza kibabe baada ya kumwamini tena Adesanya katika mechi ya marudiano na Pereira Jana Jumamosi usiku huko Miami.

Drake aliweka dau la $500,000 kwa Adesanya kushinda na kujishindia $885,000 lakini pia aliweka dau la $400,000 ili ashinde kwa KO na kujikusanyia dola milioni 1.8 ambapo jumla ameshinda takribani dola milioni 2.7

Chanzo: www.tanzaniaweb.live