Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dodoma Jiji waanza maandalizi ya Ligi Kuu

05c90e2f811e8b07c2b6a3aaa9fd4b45 Dodoma Jiji waanza maandalizi ya Ligi Kuu

Wed, 22 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MABINGWA wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL), Dodoma Jiji wameanza maandalizi ya kujipanga kwa ajili ya kuleta ushindani kwenye mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu mpya wa mwaka 2020/2021.

Dodoma walitwaa ubingwa huo kwa kuifunga Gwambina FC kwa bao 1-0 katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Dodoma walipanda Ligi Kuu baada ya kufanya vizuri kwenye Kundi A lililokuwa linajumuisha timu 12 na Gwambina wamepanda kutoka Kundi B wakiongoza kwa pointi nyingi sana.

Benchi la ufundi la timu hiyo kupitia kwa kocha wao Mbwana Makata alisema maandalizi hayo ni pamoja na kusajili wachezaji wapya ambao wana uzoefu kwenye michezo ya ligi ili kutengeneza kikosi kitakacholeta ushindani.

“Kazi ya kwanza tulishamaliza ya kutoka sehemu ngumu tena kwa ushindani mkali na tulifanikiwa kuongoza kundi kwenye mechi ya mwisho kutokana na changamoto ya kundi letu, sasa tunajipanga kusajili wachezaji wapya kutengeneza kikosi chetu," alisema Makata.

Makata alisema ni wanahitaji kufanya maandalizi makubwa kwa kuwa wanaingia kwenye ligi iliyosheheni timu nyingi zilizowekeza kwa kuwa na wachezaji wazuri.

Naye nahodha wa kikosi hicho, Hamisi Kibacha aliyewahi kuichezea timu ya Coastal Union amesisitiza kuonesha mfano kwenye ligi na kutamba ushindani wa Ligi Kuu ni mdogo ikilinganishwa na daraja la kwanza.

“Tukiwa Daraja la Kwanza, tumecheza mechi nyingi za kirafiki na timu za Ligi Kuu na tulikuwa tunapata ushindi mzuri, naamini maboresho ya kikosi yatakayofanyika kwa maingizo ya wachezaji wapya, tutatoa ushindani mkubwa,” alisema Kibacha.

Hadi sasa Dodoma wameungana na Gwambina FC, waliotoka kundi B kushiriki Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu ujao huku wakisubiri michezo ya play off ambayo itatoa timu nyingine mbili.

Chanzo: habarileo.co.tz