Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dkt.Mshindo Msola awapa ukweli wana Yanga

Yangasc 144820179 860528904768367 719982656233316999 N Dkt.Mshindo Msola awapa ukweli wana Yanga

Mon, 8 Nov 2021 Chanzo: eatv.tv

Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Dokta Mshindo Msola amesema kuwa kila Mwanachama wameridhia kulipia 31000 ili kupata kadi ya uanachama ili kusaidia kuiendesha timu yao.

Msolla ameyasema hayo wakati akizungumza na East Africa Radio katika ziara ya Rais wa Mashabiki, Goza Chuma ambaye wiki iliyopita alitembelea ofisi za timu hiyo ili kujua maendeleo ya mabingwa hao wa kihistoria wa Ligi Kuu Tanzania bara.

Dokta Msoll amesema kuwa Wanachama ndio wawekezaji namba moja wa timu huku akisisitiza kuwa hakuna Mwekezaji makini anayeweza kuwekeza katika klabu yenye madeni na isiyoweza kujiendesha.

''Niwaambie Wana Yanga nchi nzima, hakuna Mwekezaji makini  atakuja leo Yanga kuwekeza, kwasababu hawezi kuweka pesa yake kwenye Klabu ambayo inadaiwa na haiwezi kujiendesha'' Dokta Mshindo Msola.

Ameongeza kuwa kwa mwenendo uliopo hivi sasa anaona kuna njia nzuri wanayoipitia kwakuwa tayari wapenzi na wanachama wameamua kuisaidia timu yao katika kujitegemea jambo ambalo litawavutia wadhamini na wawekezaji.

Chanzo: eatv.tv