Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dk Ndee: RT hakukuwa na ushirikiano

211a8fc365dec79cc73396c490434a62.png Dk Ndee: RT hakukuwa na ushirikiano

Mon, 25 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

MAKAMU wa Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Dk Hamad Ndee amesema kuwa kikubwa alichoki na katika uongozi wao wa miaka minne ndani ya RT ni ukosefu mkubwa wa ushirikiano.

Akizungumza katika mahojiano maalum , Ndee ambaye ni muhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alisema hivi karibuni kuwa mambo mengi yalishindwa kufanyika ndani ya shirikisho hilo sababu ya kutokuwa na ushirikiano.

Alisema kuwa hajaridhika kabisa na maendeleo ya mchezo huo nchini katika kipindi cha miaka minne iliyopita kwani viongozi walikosa ushirikoano na kushindwa kuinua mchezo huo.

Akizungumzia kuhusu ukiukwaji mkubwa wa Katiba ya shirikisho hilo kwa kutofanya baadhi ya mikutano kama ilivyotakiwa, Ndee alikiri hilo na kusema wanaohusika walishindwa kuitisha vikao.

Alisema yeye ni Makamu wa Pili wa Rais na jukumu lake kubwa ni kushighulikia masuala ya ufundi na alihakikisha hilo linafanyika na kila mwaka aliiweka mashindano ya taifa na mengine katika kalenda, lakini hayakufanyika.

“Kweli kulikuwa na ukiukwaji mkubwa wa Katiba kwa kutofanya vikao na mashindano kama Katiba ilivyoeleza, lakini mimi niliwajibika kwani kila mwaka nilipanga ratiba na kuiweka katika kalenda yetu, lakini wahusika walidai hakuna fedha na hilo sio jukumu langu, “alisema Ndee.

Ndee ambaye anagombea Umakamu wa Rais, ambao sasa atakuwa mmoja baada ya mabadiliko ya Katiba alisema amechukua fomu ili jyusaidia RT katika suala zima la ufundi kwani yeye ni mtaalam katika hilo.

Alisema kuwa makocha wa riadha ni wachache na hata waliopo hawana viwango baada yakutokuwa na elimu ya kutosha ya mchezo huo, hivyo anataka kusaidia kutoa mafunzo ili kupata makocha wengi zaidi watakaoibua vipaji na kuviendeleza.

Alisema kuna uhaba mkubwa wa makocha wa riadha na waliopo hawako katika viwango kwani hawajapata mafunzo ya kutosha kwa ajili ya mchezo huo, hivyo hawajui wafanye nini.

Dk Ndee mbali na uongozi, pia alikuwa mwanariadha wa mbio za meta 200 fupi na kushiriki Michezo ya Olimpiki ya Munich, Ujerumani 1972 na sasa ni kocha anayetambuliwa na Riadha ya Dunia (WA).

Uchaguzi Mkuu wa RT umepangwa kufanyika Januari 30 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa ukitanguliwa na usaili Januari 28.

Msemaji wa RT, Tullo Chambo alipoulizwa kuhusu madai ya Ndee kutokuwepo kwa ushirikiano alisema aulizwe kaimu katibu mkuu, Ombeni Zavalla, aliyepigiwa simu mara kadhaa, hakupokea.

Chanzo: habarileo.co.tz