Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Djokovic awashusha presha mashabiki

Novak Djokovic Walter Gwiji wa Tennis Novak Djokovic

Thu, 6 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Gwiji wa Tennis Novak Djokovic amethibitisha kufanyiwa upasuaji wa goti kwa mafanikio, baada ya kujitoa kwenye michuano ya French Open.

Mserbia huyo amethibitisha habari hizo kwenye ukurasa wake wa Mtandao wa Kijamii wa Instagram akiandika: "Siku kadhaa zilizopita, nililazimika kufanya maamuzi magumu baada ya kupata majeraha wakati wa mechi yangu ya mwisho. Nina furaha kuwajulisha kwamba upasuaji ulikwenda vizuri.

"Ninashukuru sana timu ya madaktari ambao wamekuwa pamoja nami, pamoja na msaada mkubwa ambao nimepata kutoka kwa mashabiki wangu.

"Nitajitahidi niwezavyo kuwa na afya njema na kufanikisha kurudi uwanjani haraka iwezekanavyo.

"Mapenzi yangu kwa mchezo huu yana nguvu na hamu ya kushindana kwa kiwango cha juu ndiyo yanayonifanya niendelee."

Chanzo: Mwanaspoti