Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ditram Nchimbi: Afuata rekodi ya Bob Choppa, Beya Simba Stars

80962 Nchimbi+pic Ditram Nchimbi: Afuata rekodi ya Bob Choppa, Beya Simba Stars

Mon, 21 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

UNASHANGAA Ditram Nchimbi kuitwa Taifa Stars baada ya kuifunga Yanga? Basi kaa ufahamu kitendo kama hicho kilishatokea katika siku za nyuma, kwa mchezaji kuchaguliwa kwenye kikosi hicho baada ya kuifunga Yanga, soma hapa chini.

Ilikuwa Mei 19, 1985 katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza (sasa Ligi Kuu) katika Uwanja wa Taifa (sasa Uwanja wa Uhuru), Dar es Salaam. Simba ilishafungwa bao 1-0. Bao la kutangulia la Yanga lilifungwa na Omar Hussein ‘Mmachinga’ katika dakika ya sita tu.

Ilionekana kama vile Simba ingelala katika mchezo ule licha ya kuwa na mastaa wake kama Zamoyoni Mogella ‘Golden Boy’ na Malota Soma ‘Ball Jugler’.

Hata hivyo, dakika ya 30, mshambuliaji asiyepewa umuhimu mkubwa na ukuta wa Yanga ukiongozwa na Allan Shomary na Athumani Juma ‘Chama’, Mohammed Bob Chopa wa Simba alipita katikati ya mabeki hao na kusawazisha bao.

Kilichofuata sasa ndio kitamu! Baada ya siku chache, Bob Chopa aliitwa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ kutokana na kitendo chake cha kuwapita mabeki wawili mahiri wa Yanga.

Bado haitoshi? Mwaka 1984 Winga wa Pamba, Beya Simba (sasa marehemu) naye aliwahi kuitwa timu ya taifa baada ya kumpita beki wa Yanga na Timu ya Taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars’ Ahmed Amasha ‘Mathematics’ mara mbili na kuipa Pamba ushindi wa mabao 2-0 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Pia Soma

Advertisement
Baada ya mchezo huo, Beya Simba alipohojiwa na waandishi wa habari aliwezaje kufunga mabao yale alijibu: Nilitumia udhaifu wa beki mahiri wa kimataifa wa Yanga ( akimaanisha Ahmed Amasha.)

Turudi kwa Nchimbi sasa. Wakati Yanga ikijiandaa na mchezo wa kimataifa dhidi ya Township ilicheza mchezo wa kirafiki na Polisi Tanzania pale Ushirika na kukubali kichapo cha mabao 2-0 yaliyofungwa na Marcel Kaheza pamoja na Ditram Nchimbi.

Nchimbi anakipiga kwenye kikosi hicho kwa mkopo akitokea Azam FC ambayo ilimnasa kutoka Njombe Mji inayotaabika kwa sasa Ligi Daraja la Kwanza (FDL) inayoendelea hivi sasa.

Oktoba 5, Uwanja wa Uhuru, alifanya yake wakati timu yake ikitoka sare ya mabao 3-3 alipotumia dakika ya 34, 55 na 58 wakati Yanga ikianza kufunga kwa bao la Mrisho Ngassa dakika ya 6, kabla ya Davidi Molinga kufunga dakika ya 65 na 68.

3- Misimu ambayo aliitumikia Majimaji FC iliyomsajili kutoka Mbinga United iliyokuwa Ligi Dara la Tatu.

3 -Idadi ya mabao aliyoyafunga mpaka sasa. Yote aliifunga Yanga.

6- Idadi ya timu za Ligi Kuu ambazo amezichezea. Alianza Majimaji FC, Mbeya City, Njombe Mji, Mwadui FC, Azam FC na sasa Polisi Tanzania.

7- Mabao aliyofunga akiwa na Njombe Mji na asisti sita.

10- Namba ya kiatu anachokivaa.

10 -Namba ya jezi aliyoivaa wakati wa mchezo wa kirafiki baina ya Rwanda na Tanzania, pia alikuwa akiivaa kule Mwadui FC na Njombe Mji.

12- Idadi ya asissti za mabao akiwa Mbeya City na kufunga mabao nane.

14 - Tarehe inayobaki kama kumbukumbu kwake akichezea kwa mara ya kwanza Taifa Stars dhidi ya Rwanda.

22- Miaka ya Nchimbi kwa sasa na ndio namba aliyokuwa akivaa Mbeya City.

2018- Mwaka ambao Azam FC ilimsajili mchezaji huyo kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Njombe Mji.

Chanzo: mwananchi.co.tz