Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dida kuchukua nafasi ya Manula

Wed, 27 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kipa namba moja wa Simba Aishi Manula alishindwa kufanya mazoezi na kipa mwenzake Deo Munishi 'Dida'.

Manula alishindwa kufanya mazoezi hayo ya ukipa chini ya kocha Muharami Mohammed 'Shilton' kwa kuwa aliumia kiganja cha mkono.

Manula aliumia mkono huo katika mechi ya Kimataifa kati ya Taifa Stars na Uganda iliyochezwa Jumapili.

Kushindwa kwa Manula kufanya mazoezi hayo Shilton alikuwa akifanya na Dida pekee yake kwani kipa namba tatu Ally Salim yupo katika timu ya Taifa.

Ni wazi Manula kushindwa kufanya mazoezi hayo Dida anapewa nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza katika mechi na Mbao ambayo itachezwa Jumapili.

Katika kuhakikisha Dida anakuwa imara na kuziba vizuri nafasi ya Manula Shilton alimpa mazoezi mengi huku akiwa anaongea nae pinda analokosea au kupatia.

Kocha wa Simba Patrick Aussems nae alikwenda alipo Dida na Shilton kusimamia mazoezi hayo na pindi Dida alipokuwa anafanya vizuri alimpongeza.



Chanzo: mwananchi.co.tz