Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dickson Job aongeza kandarasi mpya Mtibwa Sugar

5819 Mtibw TZW

Thu, 5 Apr 2018 Chanzo: bongo5.com

Beki kisiki wa timu ya vijana wa Mtibwa Sugar SC, Dickson Nickson Job ameongeza mkataba wa miaka mitatu kuendelea kutumikia kikosi cha wana tam tam.



Dickson Nickson Job (Katikati) akisaini mkataba mbele ya mkurugenzi wa Mtibwa Sugar Sc Jamal Bayser na George Job.

Beki huyo kinda, Job aliambatana na kaka yake, George Job anayemsimamia katika masuala ya mpira ili kumuongoza kijana huyo na sheria zinamtaka kijana mwenye umri huo kuwa na msaidizi katika kuingia  mkataba.



Nickson Job ambaye ni Captain wa timu ya vijana ya Mtibwa Sugar na timu ya taifa ya vijana “Ngorongoro heroes” ameongezewa makataba huo kutokana na kiwango alicho kionesha na viongozi wa Mtibwa Sugar wametoa ahadi ya kuendelea kuwa amini vijna.

Dicskon Job alikuwa ametumikia kikosi cha Mtibwa Sugar kwa miaka 2 na miaka yake miwili ilikuwa yenye ushawishi mkubwa kwa wana Mtibwa Sugar  hivyo kuamua kumpatia mkataba mpya wa miaka 3.

Chanzo: bongo5.com