Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dharau za Sanchez kwa Chelsea zavuka mipaka

1039 47B3366000000578 5231115 Image A 5 1514970875513 TZW

Thu, 4 Jan 2018 Chanzo: bongo5.com

Wakati klabu ya Arsenal ikijiwinda dhidi ya Chelsea, mchezaji wake, Alexis Sanchez ameonekana kutokuwa na presha kabisa na mchezo huo baada ya kuonekana akiwa katika gari aina ya ‘tractor’ na mwenye furaha pasipo hofu.

Alexis Sanchez akifanya masikhara wakati wachezaji wenzake wa Arsenal wakifanya mazoezi

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Chile, Sanchez ameonekana mwenye kujiamini huku akishuka kutoka katika ‘tractor’ mbele ya kamera za Arsenal wakati wenzake wakiwa katika mazoezi kana kwamba anauhakika wa kushinda mchezo wao dhidi ya Chelsea.

Mchezaji huyo wakimataifa wa Chilean akiigiza anaendesha gari aina ya tractor  wakati kikosi cha Arsenal kikijiandaa na mchezo dhidi ya Chelsea

Mbali na maskhara yaliyokuwa yakifanywa na Sanchez, mazoezi yamezidi kuendelea ili kujiimarisha zaidi  chini ya kocha , Arsene Wenger.

Katika kikosikilichokuwepo mazoezini ni pamoja na wachezaji wazoefu kama, Jack Wilshere, Danny Welbeck na Theo Walcott wakati vijana wengine ni Joe Willock, Ainsley Maitland-Niles na Eddie Nketiah.

Chanzo: bongo5.com