Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Deo Kanda aitaka Yanga Uwanja wa Taifa

90352 Kanda+pic Deo Kanda aitaka Yanga Uwanja wa Taifa

Tue, 31 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mshambuliaji wa Simba Deo Kanda  amesema bao alilofunga Jumamosi dhidi ya KMC ni salamu kwa Yanga y watakutana Januari 4 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Taifa. Kanda ambaye ni mchezaji wa TP Mazembe ya DR Congo anayecheza Simba kwa mkopo, alisema hana presha ya kucheza mchezo wa watani wa jadi. Mchezaji huyo alisema ana uzoefu wa kutosha na michezo ya watani wa jadi tangu akiwa DR Congo na Morocco. “Nasubiri ndio mchezo ambao naweza kuonyesha uwezo wangu mashabiki wetu watakuwa wakitushangilia siwezi kuwa tayari kuwaangusha najiona  niko katika kiwango kizuri. “Nikiwa nyumbani DR Congo niliwahi kucheza michezo ya namna hii zaidi ya mara tano. Kuna mechi ya Lubumbashi  kati ya TP Mazembe  dhidi ya  FC Lupopo,” alisema Kanda. Pia aliwahi kucheza Vita Club na DC Motema Pembe kwa vipindi tofauti ambao ni wapinzani. Kanda aliwahi kucheza Raja Casablanca ambao wapinzani wao wakuu ni  Wydad Athletic katika Ligi ya Morocco. Kanda ameifungia Simba mabao mawili msimu huu, moja katika ligi dhidi ya KMC ambapo aliisaidia klabu yake kuibuka na ushindi wa mabao 2-0. Winga huyo alifunga bao jingine katika mchezo wa mashindano ya Kombe la FA dhidi ya AFC Arusha. Simba ilishinda mabao 6-0 kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na kuitupa nje.

Chanzo: mwananchi.co.tz