Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dawasa FC waichabanga Moruwasa

Moro Pic Data Dawasa FC waichabanga Moruwasa

Mon, 17 May 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

MOROGORO. Timu ya soka ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira ya Jijini Dar es Saalam, Dawasa FC imejitangazia ubabe na umwamba kwa timu za mamlaka hiyo chini ya Wizara ya Maji baada ya kutembeza kipigo cha bao 5-2 dhidi ya wenye wao Moruwasa FC ya mkoani Morogoro wakati wa mchezo mkali wa kirafiki uliofanyikwa katika uwanja wa Highland Bigwa mkoani hapa. Mchezo huo uliozikutanisha timu hizo ilikuwa na lengo la kudumisha umoja na ushikamano na kubadilishana mawazo ya kiutendaji kazi ya kuhudumia wananchi baina ya mamlaka hizo mbili lakini ikiacha manung’uniko na huzuni kwa wenyeji. Ubabe, umwamba kwa timu ya Dawasa FC kumetokana na kipaji kilichoonyeshwa nashambuliaji wao, Prosper Nyagawa kwa kufunga bao tatu pekee yake katika mchezo huo huku Abdalah Sokolo, Amos Mjemla wenyewe wakifunga bao moja moja katika ushindi huo. Wenyeji walipata bao za kufutia machozi baada ya mchezaji tegemeo wa Moruwasa, William Komba kufunga bao mbili pekee yake katika mchezo.

MOROGORO. Timu ya soka ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira ya Jijini Dar es Saalam, Dawasa FC imejitangazia ubabe na umwamba kwa timu za mamlaka hiyo chini ya Wizara ya Maji baada ya kutembeza kipigo cha bao 5-2 dhidi ya wenye wao Moruwasa FC ya mkoani Morogoro wakati wa mchezo mkali wa kirafiki uliofanyikwa katika uwanja wa Highland Bigwa mkoani hapa. Mchezo huo uliozikutanisha timu hizo ilikuwa na lengo la kudumisha umoja na ushikamano na kubadilishana mawazo ya kiutendaji kazi ya kuhudumia wananchi baina ya mamlaka hizo mbili lakini ikiacha manung’uniko na huzuni kwa wenyeji. Ubabe, umwamba kwa timu ya Dawasa FC kumetokana na kipaji kilichoonyeshwa nashambuliaji wao, Prosper Nyagawa kwa kufunga bao tatu pekee yake katika mchezo huo huku Abdalah Sokolo, Amos Mjemla wenyewe wakifunga bao moja moja katika ushindi huo. Wenyeji walipata bao za kufutia machozi baada ya mchezaji tegemeo wa Moruwasa, William Komba kufunga bao mbili pekee yake katika mchezo. Akizungumza baada ya mchezo huo kumalizika mkoani hapa Mkuu wa idara ya biashara Moruwasa, Kiguhe Liang’onjo aliwapongeza wapinzani wao kwa ushindi huo. Liang’onjo alisema kipigo walichopata wachezaji wake hakitawakatisha tamaa na wanajipanga kutoa ushirikiano kwa mamlaka nyingine kuona kama wanaweza kucheza nao katika mpango wa kukusanya uzoezi ili kuongeza mshikamano na ufanisi wa kazi yakuwahudumia wateja wao kupitia michezo. “Tumekutana hapa wote sisi  kama taasisi ya wizara ya maji kwa ajili ya kuburudika nakubadilishana mawazo kulingana na huduma zetu tunazozitoa kwa wananchi ilituweze kuboresha hutoaji wa huduma bora kwa jamii inayo tuzunguka licha ya wenzetu mmetukamia na kutufunga bao 5-2 sisi tunajipanga tulipize kisasi,” alisema Liang’onjo. Kwa upandewa kocha wa Moruwasa, Sadiki Singano alisema sababu ya timu yeke kupoteza mchezo huo imetokana na timu yake kuwa na muda mfupi wa mandalizi tofauti nawapinzani wao ambao wameimalika kila idara. Singano alisema kuwa katika kipigo hicho amejifunza mbinu tofauti tofauti kutoka kwa mpinzani wake na kwenda kuzifanyia kazi ili wawe bora katika michezo ijayo ikiwemo kuwa na michezo ya kirafiki ya mara kwa mara itayosaidia kujenga timu yenye uzoefu. Nahodha wa Dawasa FC, Elias Kelenge alisema kuwa wamefanya maandalizi ya kutosha yakujiandaa na mchezo huo na imekuwa rahisi kwao kutekeleza maagizo ya benchi lao la ufundi. “ Mazoezi ndiyo siri kubwa ya ushindi huu tunafanya sana mazoezi na kujituma uwanjani umeona hamasa kutoka kwa mashabiki tuliotoka nao Dar es Saalam hata wachezaji kucheza kwa kwa bidii kwa ajili ya timu yetu” alisema Kelenge.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz