Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dawa ya washambuliaji Yanga, Simba

73684 DAWA+PIC

Mon, 2 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2019/2020 umeanza rasmi ambapo tumeshuhudia timu 20 zikiumana katika viwanja mbalimbali kuwania pointi tatu muhimu.

Jicho la wengi lilielekezwa hapa jijini Dar es Salaa ambako timu za Simba, Yanga, Azam FC na KMC zilizomaliza kwa kwenye nafasi nne za juu zilitupa karata zao za kwanza.

Azam ilianza siku ya Jumanne kwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya KMC na Jumatano, Yanga ilijikuta ikipoteza mbele ya Ruvu Shooting kwa bao 1-0 na mechi ya juzi Alhamisi, tulishuhudia Simba ikiibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya JKT Tanzania.

Mechi hizo zote zilichezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini.

Hata hivyo pamoja na ushindani ulioonyeshwa kwenye mechi hizo, safu za ushambuliaji za vigogo viwili vya soka nchini, Yanga na Simba zilionyesha udhaifu mkubwa wa kutumia nafasi ambazo timu hizo zilitengeneza.

Yanga licha ya kumiliki mpira dhidi ya Ruvu Shooting ilishindwa kupachika bao hata la kuotea lakini Simba ingawa iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 nayo ilipoteza nafasi nyingi za wazi ambazo kama ingezitumia vizuri basi zingewafanya waibuke na ushindi mnono kwenye mechi hiyo.

Pia Soma

Advertisement   ?
Takwimu zinaonyesha kwamba Yanga ilipiga mashuti tisa (9) yaliyolenga lango lakini yote hayakuzaa matunda wakati Simba ilipoteza nafasi takribani tano za wazi.

Kiujumla tatizo hili la kupoteza nafasi kwa washambuliaji linachangiwa kwa kiasi kikubwa na ukosefu wa utulivu wa washambuliaji hao kwenye eneo la hatari la timu pinzani.

Pindi mechi inapochezwa kunakuwa na mambo mawili ambayo ni ‘defending phase’ na ‘offending phase’ (nyakati ya kushambulia na nyakati ya kujilinda au kuzuia).

Pindi timu inapokuwa na mpira, wazo huwa ni kushambulia, hivyo itahakikisha inatafuta namna ya kwenda kushambulia, hii ndio tunaita offending phase.

Lakini pale inapoupoteza, kila mchezaji akili yake inapaswa kuwa kwenye kuusaka mpira, hii ndio tunaita ‘defending phase’.

Sasa inapoupata mpira, inafanya kitu kinaitwa ‘transitional movement’ ambayo inahusisha vitu kadhaa vikiwemo ‘depth, mobility na penetration.

‘Penetration’ ni kupasua ukuta wa wapinzani na kuingia kwenye eneo lao na pindi mnapofanya hivyo kila mchezaji anapaswa kukaa kwenye nafasi sahihi na ndio maana kuna ulazima wachezaji kufanyia kazi mazoezini hilo ili pindi timu inapojaribu kupenya, mpira umkute akiwa kwenye eneo husika.

Na hapa kuna mambo matatu ambayo yatafanikisha hilo ambayo ni uwezo binafsi wa mchezaji mmojammoja au tunaita ‘positional play’, uwezo wa kitimu au idara husika.

Sasa wachezaji wa Simba na Yanga wanakosa ‘concentration na anticipation’ pindi wanaposhambulia hivyo mchezaji anajikuta anashindwa afanye nini pindi mpira unavyomkuta akiwa langoni. Kikubwa kinachotakiwa kufanyika ni makocha kufanya ‘performance analysis’ (tathmini ya utendaji kazi) ambayo itahusisha mambo matano.

Kwanza ‘observation’ ambayo ni kuona tatizo lakini pili ni kufanya ‘analysis’ (uchambuzi) wa kujua wanafeli wapi na jambo la tatu ni ‘interpretation’ (kutafsiri tatizo).

Kinachofuatia ni ‘planning’ (kupanga nini cha kufanya) na baada ya hapo ni kufanya jambo linaitwa ‘preparation and ammendment’ (maandalizi na utekelezaji)

Chanzo: mwananchi.co.tz