Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Daktari azua kituko Olimpiki 2024

Tdxtfxch Daktari azua kituko Olimpiki 2024

Thu, 1 Aug 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Olimpiki kuna vituko vyake. Kama hiki. Daktari mmoja amejikuta akigeuka gumzo kwenye mitandao ya kijamii baada ya kujikuta amekalia kiti cha mchezaji mgonjwa.

Kituko hicho kilitokea wakati wa mchezo wa mapanga kati ya Nathalie Moellhausen wa Brazil dhidi ya Ruien Xiao kutoka Canada Jumamosi iliyopita na Moellhausen alianguka na madaktari wawili waliwahi kumsaidia.

Ripoti zinaeleza mchezaji huyo alikuwa na uvimbe uliomsababishia maumivu na madaktari hao Wabrazil waliwahi kumpa huduma ya kwanza na ndipo kiti kilipoletwa kwa ajili ya mgonjwa, daktari mmoja akakikalia akidhani alipewa yeye akae ili amtibie mchezaji.

Hata hivyo, baada ya kukaa, mhudumu aliyeleta kiti alimshtua sio chake na haraka alisimama na kuendelea kumpa huduma mchezaji huyo.

Huko kwenye mitandao ya kijamii na hasa wa X, mashabiki hawakumuacha salama kutukana na kituko hicho na waliandika maoni yao, na mmoja alisema inawezekana daktari huyo alijaribu kukaa ili kuhakikisha kama kiti kilikuwa imara, mwingine akasema "Alikuwa anakipa joto kwani kulikuwa na baridi."

Baada ya kudondoka, Moellhausen alifikishwa Hospitali na akafanyiwa upasuaji Jumatatu.

Inadaiwa uvimbe huo uligunduliwa Februari mwala huu, lakini Moellhausen hakufanyiwa upasuaji hali iliyoendelea kumsababishia maumivu makali kiasi cha kulazwa muda mfupi kabla ya michezo ya Olimpiki kuanza na inaaminika alichomwa sindano za kutuliza maumivu ili kushiriki michezo hiyo.

Chanzo: Mwanaspoti