Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dakika 90 zilivyobadili maisha ya kiungo Makame Yanga

77029 Makame+pic

Tue, 24 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Abdulaziz Makame hakuwa maarufu, lakini dakika 90 alizocheza katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zesco ya Zambia, zimemtambulisha rasmi.

Hakuna aliyetarajia kama Makame atacheza kwa kiwango cha juu kwa kuwa hakuwemo katika akili za mashabiki wa klabu hiyo.

Idadi kubwa ya mashabiki wa Yanga huwaelezi kitu kuhusu mastaa wao akina Patrick Sibomana, Juma Balinya na beki kisiki Lamine Moro waliosajiliwa msimu huu.

Makame aliyejiunga na Yanga akitokea Mafunzo ya Zanzibar, hakuwa akitajwa sana na mashabiki hao kama ilivyo kwa Sibomana au Balinya wanaocheza kikosi cha kwanza.

Hata pale Kocha Mwinyi Zahera alipoliweka jina la Makame katika orodha ya wachezaji wa kuanza dhidi ya Zesco, baadhi ya mashabiki waliibua mjadala.

Wapo mashabiki waliodhani Zahera anacheza kamari kumpanga Makame katika mchezo mgumu ambao Yanga haikuwa na namna zaidi ya kupata ushindi.

Pia Soma

Advertisement
Pamoja na minong’ono hiyo Zahera alisimamia msimamo wa kumpa nafasi mchezaji huyo kutoka Zanzibar, kwa kuwa aliamini ana kipaji cha soka.

Lwandamina afunguka

Mchezaji huyo amemvutia Kocha wa Zesco George Lwandamina ambaye amemtaja Makame ni hazina ya Yanga na timu ya Taifa, ‘Taifa Stars’.

Lwandamina anasema Makame ni kiungo mwenye kasi na mchezaji anayeweza kutekeleza vyema maelekezo ya benchi la ufundi anapokuwa uwanjani.

Kocha huyo anasema katika mchezo wao, alitibua mipango mingi baada ya kumiliki kwa ufasaha eneo la katikati alilodai ndio mhimili wa Zesco.

“Yule kijana (Makame) ni hodari, alichangia kiasi kikubwa tusipate mabao kwasababu alimudu kuwazima wachezaji wangu wa katikati. Ni mmoja wa wachezaji walionivutia Yanga,” anasema Lwandamina.

Kiungo huyo anasema ni sifa kubwa kusifiwa na kocha bora kama Lwandamina kwa kuwa inaonyesha namna anavyokubali kazi yake uwanjani. “Mpira ni kazi yangu na moja ya ndoto zangu ni kucheza soka la kulipwa nje ya nchi, kwahiyo siwezi kukataa nafasi ya kufanya kazi, na Lwandamina, lakini nitaondoka Yanga kwa utaratibu mzuri kwa muda sahihi,” anasema Makame.

Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam , Yanga ilikuwa wa kwanza kupata bao kwa mkwaju wa Penalti, lililofungwa na Patrick Sibomana kabla ya Thabani Kamusoko kusawazisha.

Makame huu ni msimu wake wa kwanza Yanga na alijiunga na timu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Mafunzo ya Zanzibar.

Kiungo huyo alianza kutema cheche katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Toto Africans ya Mwanza ambapo alifunga bao kwa kiki kali.

Zesco

“Nilivyoona nitaanza katika kikosi cha Yanga nilifurahi kwa sababu niliona ule muda ambao nilikuwa nikisubiri kwa muda mrefu. Nilitaka kuonyesha na kumuaminisha kocha awe ananipa nafasi ya kucheza mara kwa mara.

“Nilikuwa nikicheza kwa maelekezo, ilikuwa rahisi kucheza katika kiwango kile kwasababu wachezaji ambao nilikuwa nikicheza nao katika eneo la kiungo nimecheza nao Zanzibar, tunajuana,” anasema Makame.

Makame anasema haikuwa kazi nyepesi kujiunga na Yanga kwa kuwa aliwahi kupita mikononi mwa watani wao wa jadi Simba ambao ni mahasimu wakubwa.

“Niliwahi kucheza Simba kabla ya kurejea Zanzibar kwa mkopo na baadaye nikaomba kuondoka. Niliona Yanga ni sehemu ambayo nitapata nafasi ya kucheza, maana ilikuwa rahisi kwangu kujiunga nayo, upande mwingine nilitaka kuungana na rafiki yangu (Feisal),” anasema.

Makame anasema AFC Leopards ya Kenya ni miongoni mwa klabu za hapa nchini zilizokuwa zikitaaa huduma yake. “Wengi hawajui niliwahi kwenda kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa Afrika Kusini katika klabu ya University of Pretoria,” anasema.

Erasto Nyoni

Makame anamtaja mchezaji kiraka wa Simba Erasto Nyoni ni mchezaji anayemvutia nchini kutokana na ubora wake wa kumudu nafasi nyingi.

Mchezaji huyo hakusita kuitaja Simba kuwa ilikuwa ndio klabu yake ya kwanza kabla ya Yanga,lakini aliondoka na kurejea Zanzibar, baada ya kukosa namba.

Chanzo: mwananchi.co.tz