Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dah! Msikie kipa huyu

Mwamunyeto Pic Data Dah! Msikie kipa huyu

Fri, 23 Apr 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

KAMA kuna kitu kimemuumiza kipa wa Gwambina FC, Ibrahim Isihaka walipocheza dhidi ya Yanga ni kufungwa bao la pili na beki Bakari Mwamnyeto dakika ya 52 ambalo amekiri lilitokana na uzembe wake.

Yanga juzi Jumanne iliichapa mabao 3-1 Gwambina FC katika Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam, jambo ambalo Isihaka anadai bao alilofungwa na Mwamnyeto lilitokana na kuwaachia kazi mabeki peke yao akijifariji kwamba wangemaliza kazi bila kumfikia.

“Katika mabao matatu niliyofungwa na wachezaji wa Yanga, nililoliona ni la kizembe ni lile Mwamnyeto, wakati mpira wa kona unapigwa niliwaangalia mabeki wangu nakuja kushtukia ulishaingia nyavuni,” alisema.

“Nadhani Yanga baada kupata bao la pili walijiamini zaidi ingawa katika safu yao ya mbele sikuona straika ambaye ni wakunipa presha ya mchezo, ni matokeo waliyotubahatisha na sio ubora wao.”

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz