Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dah! Kumbe moyo wa Chilunda unauvimbe

61089 Pic+chilunda

Mon, 3 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Pamoja na klabu yake ya Azam FC kutaka kumrudisha nyumbani mshambuliaji Shaban Idd Chilunda amebainika moyo wake unauvimbe.

Kwa mujibu wa tovuti ya klabu CD Tenerife mapema mwezi uliopita iliripoti kuwa walifanya majadiliano na CD Izarra iliyokuwa ikimtumia kwa mkopo pamoja na Azam juu ya hatma ya nyota huyo.

Chilunda alitakiwa kwenda Tenerife kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya chini ya jobo la madaktari wa CD Tenerife.

Vipimo vya awali vilionyesha kuna uvimbe katika moyo wake ‘acute pericarditis’ hivyo alitakiwa kufanyiwa matibabu yake mjini Tenerife.

Pia, kuwekwa chini ya uangalizi pamoja na jinsi matibabu yatakavyofanyika kuanzia mwanzo hadi mwisho.

Klabu hizo tatu zimejulishwa juu ya suala hilo na kuona jinsi watakavyoweza kutoa uamuzi wa mwisho kabla ya kuanza matibabu rasmi.

Pia Soma

Hata hivyo, Juni mosi klabu yake ya Azam FC ilishindwa kufikia makubaliano na CD Tenerife juu ya mshambuliaji huyo kubaki kwa msimu kwa 19/20.

Chipukizi huyo wa Tanzania alijiunga na CD Tenerife msimu wa 2018/19 na kufanikiwa kucheza mechi tatu za ligi kabla ya kutolewa kwa mkopo kwa CD Izarra (ya daraja la pili B).

“CD Tenerife inachukua nafasi hii kumtakia Chilunda mafanikio mema ya maisha yake kisoka na binafsi,” ilisema taarifa ya klabu hiyo.

Chilunda kwa sasa amerejea nchini akiwa katika kikosi cha Tanzania ‘Taifa Stars’ wakijianda na mashindano ya Afcon, Misri.

Chanzo: mwananchi.co.tz