Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC Jerry Muro awaombea pesa Yanga kwa tajiri Mo

9992 PIC+JERI TanzaniaWeb

Sat, 4 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

KILA inapofika Agosti 8, Simba wanafanya sherehe ya siku ya kuanzishwa kwa klabu hiyo, jambo lililosababisha aliyekuwa msemaji wa Yanga, Jerry Muro ambaye kwa sasa ni DC wa Arumeru kufunguka jambo.

Muro aliandika ujumbe huu kwenye mtandao wa kijamii kwamba "Kuelekea tamasha la simba day tunapaswa kujifunza mengi kutokana na tamasha hilo la watani wetu wa jadi, kwanza kabisa tunapaswa kujifunza uzalendo wa kupenda vyetu na kusaidia wenzetu pindi msaada unapohitajika.

"Watani zetu simba nawapongeza kwa kuanzisha tamasha hilo" simba day" kwani mmeonesha uzalendo mkubwa sana kwa timu yenu kwa kupitia tuzo mbalimbali mnazotoa kwa waliowahi kuitumikia klabu yenu yaani waasisi, hii inatia moyo kwa wachezaji na viongozi wenu kuweza kujituma ili kuipa simba mafanikio makubwa,"alisema.

Aliendelea kutiririka na kusema kuwa " pia kwa misaada mbalimbali mnayotoa kwa wahitaji kama vile yatima na wasiojiweza ni kitu muhimu sana kwa maisha ya kawaida ya kibinadamu na hili ndilo hasa lililonifanya niandike makala hii.

"Napenda kuwashauri viongozi wa Simba pamoja na mwekezaji wao bwana Mo Dewji,  kwamba msaada huo uelekezwe kweli kwa wahitaji na si kutoa kwa wasiokuwa na uhitaji wa msaada huo,"alisema.

Lakini pia katika ujumbe huo, alimuomba Mo kwamba si vibaya akiwasaidia watani wake Yanga ambao wanapita katika kipindi kigumu cha ukata.

"Kipaumbele changu katika msaada huo ni yatima na wasiojiweza na kama bwana Mo akiwa vizuri zaidi ni vyema pia akawapatia msaada wa kipesa watani wake Yanga,  japo milion 100 kwani hiyo ni pesa ndogo sana kwake,  kijana huyo wa  Afrika, lakini kwetu sisi  Young Africans ni kiasi kikubwa sana kutokana changamoto ya ukata wa pesa tunayopitia.

"Na akifanya hivyo hatutomsahau maishani, japo utani wa Simba na Yanga utaendelea milele,  lakini Mungu atambariki kwa kuwa na moyo wa kusaidia wahanga mbalimbali,"alisema DC Muro msemaji wa zamani wa Yanga.

Chanzo: mwananchi.co.tz