Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Cristiano Ronaldo amfuata Mohamed Salah Misri

5150 4A5E851E00000578 0 Image A 24 1521552891309 TZW

Wed, 21 Mar 2018 Chanzo: bongo5.com

Mchezaji bora duniani na mshindi mara tano wa tuzo za Ballon d’Or, Cristiano Ronaldo amejiunga na kikosi cha timu yake ya taifa ya Ureno katika kambi yao iliyopo nje kidogo na mji mkuu wa Lisbon tayari kujiandaa na mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Misri ambayo anatoka nyota hatari kwa sasa ulimwenguni anayekipiga ndani ya klabu ya Liverpool ya nchini Uingereza, Mohamed Salah.



Ronaldo akiwa na timu yake ya taifa ya Ureno atacheza na mafarao hao siku ya Ijumaa ikiwa ni sehemu ya maandalizi yao kwaajili ya michuano mikubwa kabisa ya kombe la dunia yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi mwezi wa sita mwaka huu nchini Urusi.



Mabingwa hao wa bara la Ulaya tayari wapo kambini Cidade do Futebol na kikosi kizima wakiwa katika mazoezi mepesi kabla ya mtanange huo

 

Baada ya mchezo wao na timu ya taifa ya Misri, Ureno watakutana na Netherlands.



Picha zikionyesha kikosi cha Ureno kikiwa kambini Lisbon

Chanzo: bongo5.com