Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

“Coutinho yuko tayari kuipamba Camp Nou”- Ujumbe wa Kampuni ya Nike

869 Coutinho TZW

Mon, 1 Jan 2018 Chanzo: millardayo.com

Deal la mchezaji wa Kimataifa wa Brazil na klabu ya Livepool Phillipe Coutinho kwenda Barcelona linaonekana  kukamilika baada ya Kampuni ya kutengeneza vifaa vya michezo ya Nike kuvujisha taarifa.

 Nike kupitia tovuti yao waliweka picha ya jezi ya Barcelona ya msimu huu yenye jina la Coutinho, huku wakiambatanisha na ujumbe unaoonyesha kuwa nyota huyo anatua Cam Nou kabla ya msimu kumalizika. “Philippe Coutinho yuko tayari kuipamba Camp Nou”, Waliandika Nike ujumbe huo kwenye picha ya jezi za FC Barcelona za msimu huu 2017-2018 iliyoandikwa jina la Coutinho.

Baadae Nike walifuta ujumbe huo baada ya mashabiki wa Liverpool kuanza kuishambulia kampuni hiyo kuwa inashinikiza mchezaji wao ahamie Barcelona kwa kuwa Nike wanaidhamini klabu hiyo ya Hispania.

BAD NEWS: JOSE MOURINHO KUHUSU HALI YA LUKAKU, BONYEZA PLAY KUTAZAMA

Chanzo: millardayo.com