Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Corona yachelewesha 'uhai' Gofu Wanawake

GOLF.jpeg Corona yachelewesha 'uhai' Gofu Wanawake

Wed, 6 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

RAIS wa Chama cha Gofu cha Wanawake Tanzania (TLGU), Sophia Reiffenstein, amesema pindi serikali itakaporuhusu michezo kurejea nchini, mikakati yao ni kuhakikisha wanafanikiwa kufufua klabu zote zilizokufa katika mchezo huo.

Serikali ilipiga marufuku shughuli zote zinazosababisha mikusanyiko ya watu nchini tangu Machi 17, mwaka huu, ikiwamo michezo kutokana na mlipuko wa maambukizo ya virusi vya corona, ambavyo vimekuwa tishio duniani kote, huku vikiendelea kuteketeza maelfu ya watu.

Akizungumza na Nipashe jijini Dar es Salaam jana, Sophia alisema wanasubiri tamko kutoka serikalini juu ya kuruhusu michezo kuendelea ili waendelee na mchakato wao wa kufufua klabu zote zilizokufa, ambao tayari walishaanza kuufanya.

Alisema hadi sasa wamefanikiwa kufufua klabu moja ya Lugalo ya jijini Dar es Salaam ambayo walifanya uchaguzi wao kabla ya janga la corona na kupata viongozi wapya.

"Sasa hivi Lugalo wanajiongoza wenyewe kwani wao walifanikiwa, ila tunasubiri mwongozo kutoka serikalini juu ya kuruhusu michezo ili tuelekee Moshi, Morogoro, Arusha na Mufindi kwa ajili ya kwenda kufufua klabu za mchezo wetu kwa wanawake," alisema Sophia.

Sophia alisema mbali na mikakati hiyo, lakini wanafikiria kuhakikisha timu ya Taifa ya Gofu ya Wanawake inaenda Namibia kushiriki michuano ya Chalenji Afrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live