Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Coastal Union yaing'ang'ania Yanga zikitoka sare

39897 Matokeo+pic Coastal Union yaing'ang'ania Yanga zikitoka sare

Tue, 5 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Timu ya Yanga imetoka sare ya bao 1-1 dhidi ya wenyeji wao Coastal Union ya Tanga kwenye mchezo wa kuvutia uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga leo Jumapili.

Matokeo hayo yanaifanya Yanga kufikisha ponti 54 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.

Sare hiyo imeiiongezea Coastal Union pointi moja na kufikisha alama 29.

Dakika 45 za mwanzo zilimalizika Coastal Union wakiwa mbele kwa bao 1-0 ingawa Yanga ndio ilionekana kumiliki mpira.

Safu ya kiungo ya Yanga ikiongozwa na Fei Toto ilikuwa imara na iliwawezesha muda mwingi mpira uchezwe muda mrefu kwenye lango la Coastal Union. Kiungo ya Coastal Union ilionekana kulemewa na kusababisha mipira ishindwe kuwafikia washambuliaji wao kwa wakati. Baada ya Coastal Union kuongoza kwa bao 1-0 ni kama utulivu ulikosekana wachezaji walikuwa wanachezeana rafu za hapa na pale na mpira kukosa utulivu.

Pamoja na Yanga kumiliki mpira kwa asilimia kubwa ilionekana kukosa utulivu ambao ulifanya washindwe kusawazisha bao kipindi cha kwanza.

Dakika ya 75 Issa Abushehe alipewa kadi nyekundu baada kumchezea rafu Michael Gadiel. Zilipita kama dakika mbili Yanga kusawazisha bao kupitia kwa Deus Kaseke baada ya kipa Casillas kutoka nje ya gori lake.

Kaseke aliamsha shangwe za mashabiki wa Yanga wakiwaacha midomo wazi wa Coastal Union kushindwa kuamini kilichotokea.

Vuruguru za hapa na pale za mashabiki zinaendelea kwenye jukwaa la mashabiki baada ya Yanga kusawazisha bao.



Chanzo: mwananchi.co.tz