Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Cioaba aifanya Azam kama Simba

82549 Pic+cioba Cioaba aifanya Azam kama Simba

Fri, 1 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

KOCHA Mkuu wa Azam FC, Aristica Cioaba ameanza kuifanya timu hiyo kama Simba baada ya kuonyesha upana wa kikosi chake katika mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Mbuni FC walioshinda 3-0. Katika mchezo huo uliopigwa jana Alhamis uwanja wa Chamazi, Cioaba alichezesha kikosi kimoja kwa dakika 45 za kwanza na dakika 45 za kipindi cha pili aliingiza kikosi kingine. Cioaba alianza kwa kuwaanzisha Razack Abarola, Nicco Wadada, Bruce Kangwa, Yakub Mohamed, Daniel Amoah, Mudathir  Yahya, Idd Seleman, Frank Domayo, Richard Djodi, Shaaban Chilunda na Idd Kipagwile. Kikosi hicho ndani ya dakika 45 kilifunga magoli mawili yaliyofungwa na Domayo pamoja na Chilunda. Kipindi cha pili alifanya mabadiliko ya kutoa kikosi chote na kuingiza kingine chini ya kipa Benedict Haule, Hama Hama, Agrey Morris, David Mwantika, Salmin Hoza, Masoud Abdallah 'Cabaye', Emmanuel Mvuyekure, Obrey Chirwa, Joseph Mahundi, Paul Peter na Donald Ngoma ambaye alifunga goli la tatu. Kwa upande wa Simba, kocha Patrick Aussems naye amekuwa akifanya mabadiliko ya mara kwa mara katika kikosi chake lakini kote amekuwa akipata matokeo. Kwa hali hii inaonyesha kwamba Cioaba ambaye amerejea Azam  wiki iliyopita anajaribu kuangalia muunganiko bora wa wachezaji wake.

Chanzo: mwananchi.co.tz