Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chuo cha Michezo Malya kutomsahau Magufuli

3ae0786af14a6669e68337267be6d412 Chuo cha Michezo Malya kutomsahau Magufuli

Mon, 22 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MKUU wa Chuo cha Michezo Malya, Richard Mganga amesema chuo hicho hakitamsahau aliyekuwa Rais John Magufuli kutokana na misaada mbalimbali aliowapatia.

Alisema katika kipindi cha utawala wa Mahufuli, chuo hicho kilitoa watalamu wengi sana katika sekta ya michezo.

‘’Rais Magufuli alisaidia sana katika uboreshaji wa miundombinu ya chuo chetu, alitenga fedha mwaka 2019/2020 kwaajili ya kuchimba visima pamoja na ujenzi wa viwanja vya michezo.’’ alisema Mganga.

Alisema Magufuli pia alisaidia chuo hicho kupangiwa fedha za maendeleo ili kuhakikisha kinazalisha watalamu wengi.

Alisema katika kumuenzi Rais Magufuli, chuo chao kitakuwa kinatoa mafunzo mbalimbali ya michezo katika mikoa tofauti ili michezo iweze kufanya vyema.

Mganga alisema katika Awamu ya Tano walifanikiwa kuanzisha kozi ya cheti kwa wahitimu wa kidato cha nne ili na wao wapate nafasi ya kufundisha na kujifunza michezo.

‘’Tumefanikiwa kuongeza ufundishaji wa michezo tisa kutoka michezo sita, pia tumeboresha mitaala ya michezo na kwa sasa tupo katika mkakati wa kufungua vituo vya michezo katika mikoa ya Dodoma na Ruvuma,’’ alisema Mganga.

Alisema tangu mwaka 2012 chuo chao hakikuwahi kupata fedha za maendeleo, lakini kupitia kwa Rais Magufuli mwaka 2019 kilipata fedha hizo na kufanya maendeleo mengi.

Alisema chuo hicho kwa sasa kipo katika mipango ya kutengeneza kituo cha kukuza na kuendelea vipaji vya vijana.

Chanzo: www.habarileo.co.tz