Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chirwa arudishwa kikosi

85840 Pic+chirwa Chirwa arudishwa kikosi

Tue, 26 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

BAADA ya kukosekana kwenye mchezo dhidi ya Mbao ambapo timu yake iliibuka na ushindi wa bao 1-0 mshambuliaji Obrey Chirwa amerudi kikosini na anatarajia kuivaa Alliance FC kesho Jumanne.

Chirwa alikosa mchezo dhidi ya Mbao kutokana na kukabiliwa na adhabu ya kadi tatu za njano sasa amemaliza adhabu hiyo na anatarajia kushuka dimbani kuisaidia timu yake kuongeza pointi tatu.

Afisa Habari wa klabu hiyo, Jaffar Idd alisema walisafiri na mchezaji huyo jijini Mwanza hivyo ni uamuzi wa kocha kumtumia au kumuacha kwenye mchezo huo.

"Chirwa anaendelea vizuri na yupo Mwanza, hakucheza mechi ya kwanza na Mbao kutokana na kuwa na adhabu ya kadi tatu za njano sasa anaruhusiwa kucheza kwa mujibu wa kanunu ni jukumu la mwalimu kumpanga au kumuacha," alisema.

Idd aliongeza kuwa wanawaheshimu wapinzani wao Alliance kuelekea mchezo huo na kwamba wamejipanga kuhakikisha wanakusanya pointi zote tatu ili kujitengenezea mazingira mazuri kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.

Timu hizo zinanatarajia kukutana zote zikiwa na kumbukumbu ya kupata matokeo mazuri michezo yao ya mwisho ambapo Azam iliifunga Mbao huku Alliance ikiipiga KMC bao 2-1.

Chanzo: mwananchi.co.tz