Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chilunda aumia mazoezini Taifa Stars

61149 Pic+mazoezi

Mon, 3 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.Mshambuliaji wa Taifa Stars, Shabani Chilunda alishindwa kumaliza mazoezi ya timu hiyo yakiyofanyika leo Jumatatu asubuhi baada ya kuumia kifundo cha mguu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Chilunda aliumia katika mazoezi hayo kifundo cha chini cha mguu wa kulia na kushindwa kumaliza mazoezi hayo na wenzake jambo ambalo madaktari wa timu walilazimika kumfunga bandeji mguuni iliyomsaidia kutembea mpaka kwenye gari la wachezaji.

Katika hatua nyingine Chilunda pamoja na klabu yake ya Azam wamefikia makubaliano na klabu yake ya kuachana na CD Tenerife ya Hispania.

Chilunda msimu huu amecheza mechi tatu katika klabu yake ya CD Tenerife kabla ya kupelekwa kwa mkopo CD Izarra.

Uongozi wa CD Tenerife ukichukua nafasi hiyo kumtakia kila la kheri huko aendapo na msimu ujao hata kuwa katika orodha ya wachezaji wa kikosi hiko.

Chilunda alisema wamefikia makubakiano na klabu yake ya CD Tenerife ya kuachana kwa amani na anaweza kwenda kujiunga na timu yoyote.

Pia Soma

"Makubaliano yetu yamekwenda vizuri na wakati huu nipo katika hatua za mwisho za mazungumzo na timu nyingine ambayo nitajiunga nayo kwa ajili ya msimu ujao," alisema.

"Timu zipo si moja ila ambayo nitakubaliana nayo nitajiunga nayo na wao ndio watakuwa na mamlaka ya kuliweka wazi jambo hili lakini kwa sasa siwezi kueleza nitakwenda timu gani.

"Suala na kurudi Azam kwa kipindi hiki ni hapana nitakuwa tena nje ya Tanzania," alisema Chilunda.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz