Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Cheka, Dulla Mbabe kukata mzizi fitina

Sat, 6 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Baada ya kukwepana muda mrefu, hatimaye mabondia nyota wa ngumi za kulipwa Francis Cheka ‘SMG’ na Abdallah Pazi ‘Dulla Mbabe’  sasa wataonyeshana umwamba Novemba 3.

Cheka na Pazi watapanda ulingoni kuwania mkanda wa dunia wa Chama Cha Ngumi za Kulipwa Cha ‘World Boxing League’ (WBL).

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, mabondia hao kila mmoja alitamba kuibuka na ushindi kutokana na mazoezi kabambe anayofanya.

Mratibu wa pambano hilo Omari Kimbau alisema abondia hao watapanda ulingoni  Uwanja wa Kinesi, kuwania ubingwa wa uzito wa super middle ukiwa ni mkanda wa kwanza kwa chama hicho kushindaniwa nchini.

Alisema mbali na Cheka na Pazi kuzichapa kwa mara ya kwanza katika historia, pia bondia kutoka Kenya, James Onyango atazipiga na Idd Pialari katika pambano la uzito wa welter ubingwa wa Afrika Mshariki na Kati.

Pia Hamisi Maya atazichapa na Habibu  Pengo katika pambano la uzito wa light wakati Salim Mtango atazipiga na Tony Rashid  uzito wa light weight. Kulwa Rashid ataonyeshana kazi na Deo Samwel uzito wa welter.

Kwa upande wa mabondia wa kike, Rehema Abdallah atazidunda na Asha Ngedere uzito wa light.  Chidi Mbishi na Sunday Kiwale watapambana katika uzito wa fly.  Pia Simba Pascal atazipiga na Imani Mpambano.

Chanzo: mwananchi.co.tz