Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chama asalimu amri kwa Azam FC

CHAMA CC Wachezaji wa Simba

Thu, 5 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa Simba, Clatous Chama 'Tripple C' amesema kuwa msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakuwa na ushindani kufuatia usajili wa wachezaji unaoendelea katika baadhi vilabu.

Chama ameyasema hayo wakati akizungumza kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram, alipogusia suala la usajili hasa katika klabu ya Azam FC iliyo chini ya kocha Mzambia George Lwandima , kuwa anaiona timu hiyo ikitengeneza kikosi bora kitacholeta ushindani msimu ujao.

"Usajili unaofanyika na Azam ni dhahiri utaleta ushindani mkubwa msimu ujao kwenye Ligi, lakini pia itakuwa poa kuona Azam ikishinda kwa ajili ya mataji na vyote unajua tusiwe tu na Ligi ya Simba na Yanga, mara hii nadhani azam FC wamesajili vizuri"

Chama alisema kuwa wachezaji wengi wanaosajiliwa na kikosi hicho anawajua na anadhani watajenga timu bora watakapokuwa na muunganiko, huku akitoa rai kuwa viongozi wanapaswa kuwa makini kwenye usajili kwani wanaweza wakasajili wachezaji wapya lakini timu ikashindwa kuwa na muunganiko mzuri.

"Suala la muunganiko ni zuri kwenye timu na unajua siyo tu suala la usajili, kwani hapa ndipo inabidi tuwe waangalifu sana kwani unaweza ukafanya usajili mpya lakini timu ikawa haina muunganiko halafu ikawa tatizo"

Azam FC mpaka sasa imenasa saini ya wachezaji saba kuelekea msimu ujao ambao ni golikipa, Ahmed Ali Suleiman 'Salula' kutoka KMKM ya Zanzibar, beki wa kushoto, Edward Manyama, kiungo mkabaji, Paul Katema (Zambia), viungo washambuliaji, Charles Zulu (Zambia), Kenneth Muguna (Kenya) na washambuliaji Rodgers Kola (Zambia) na Idriss Mbombo (DRC).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live