Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chama akataa mke

32955 Pic+chama Tanzania Web Photo

Sat, 22 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

UKISIKIA mahaba niue ndio haya. Unaambiwa shabiki  mmoja  wa Simba alikuwa tayari kumtoa mke wake pamoja na hali ya hewa kuna hatarishi kwa Clatous Chama kama angempa jezi. Jamaa amekuwa gumzo kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii na bango analotajwa kuingia nao kwenye mchezo uliopita wa Ligi Kuu Bara ambao Simba iliifunga KMC mabao 2-1 pale uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Bango hilo lilikuwa likisomeka kwa lugha ya kiingereza kuwa Chama ambaye ni raia wa Zambia akimpa jezi yake basi na yeye atatoa zawadi ya mke wake kwa fundi huyo. Ujumbe huo, umemstua Chama ambaye ameibuka kupita ukurasa wake wa Intagram na kuandika atatoa zawadi ya jezi yake kwa shabiki huyo, lakini hatokuwa tayari kumchukua mke wake. Chama aliomba msaada kwa wafuasi wake kwenye mtandao kuwa anahitaji kumpata shabiki huyo ili ampatie jezi yake yenye namba 27 mgongoni kama alivyohitaji shabiki huyo wa kutupwa wa wekundu wa Msimbazi, Simba. “Namtafuta huyu jamaa, kuna jezi yake nimemuandalia ingawa sitamchukua mke wake, nisaidieni kuwa-tag rafiki zako nao wawa-tag rafiki zao au 'repost' posti hii mpaka tumpate na kumtimizia ndoto yake,” aliandika Chama kwenye ukurasa wake. Kiungo huyo, alisema anafurahia maisha ya Tanzania kwa namna ambavyo mashabiki wanavyoonyesha upendo wao kwake na akasema atahakakikisha anaendelea kuitumikia Simba kwa uwezo wake wote. Chama alijunga Simba mwanzoni mwa msimu huu akitokea Zambia kwenye klabu ya     Lusaka Dynamos FC.

Chanzo: mwananchi.co.tz