Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chama aanza kuchonga Mashujaa

Tue, 13 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Kocha wa Mashujaa FC, Rashid Chama amesema hawatarajii kuacha pointi tatu katika mechi zilizobaki za Ligi Daraja la Kwanza.

Kauli ya Chama imekuja muda mfupi baada ya Mashujaa kuilaza Mgambo Shooting mabao 2-0, katika mchezo uliochezwa juzi.

Timu hiyo ya mkoani Kigoma kabla ya mchezo wa juzi, ilicheza mechi tatu mfululizo sawa na dakika 270 bila kupata ushindi  zaidi ya kufungwa.

Akizungumza jana, Chama alisema mechi zilizobaki zitakuwa fainali kwao kwa kuwa lengo lao ni kujiweka katika mazingira mazuri ya kupanda Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kocha huyo alisema makosa waliyofanya katika mechi zilizopita walizocheza ugenini viwanja vya ugenini wamerekebisha na matarajio yake ni kupata matokeo mazuri.

“Tumeshtuka lazima tupambane kuhakikisha mechi zilizobaki tunashinda, tulijichanganya katika michezo iliyopita hasa ya ugenini na kupoteza michezo yote, kwahiyo tumejipanga  kushinda,”alisema Chama.

Chama ameomba wadau na mashabiki wa klabu hiyo mkoani Kigoma kuwaunga mkono wachezaji wa Mashujaa ili kufikia malengo.

“Mashabiki na wadau wa soka tuungane kwa pamoja kuisapoti timu yetu ili kuweza kuisaidia kufikia malengo, benchi la ufundi tumejipanga kufanya kazi vizuri,”alisema kocha huyo.

Mashindano ya Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara, yameshika kasi kwenye viwanja tofauti mikoani.



Chanzo: mwananchi.co.tz