Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chama, Okwi, Kagere waichakaza Mbabane Swallows

30168 Pic+zima TanzaniaWeb

Wed, 5 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Manzini. Simba hawakukosea kusajili kikosi cha mauaji kimataifa na ndivyo ilivyokuwa kwa washambuliaji wake. Cletous Chama, Meddie Kagere akiunganisha nguvu na Emmanuel Okwi na John Bocco waliokuwepo.

Iko hivi. Wachezaji hao, Chama na Kagere, mchezo wa kwanza waliwafunga bao moja kila mmoja na jana wakaifungia tena Simba ikishinda 4-0 mchezo wa marudiano Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mbabane Swallows kwenye Uwanja wa Somhlolo.

Kati ya mabao manne, Chama alifunga mawili wakati Kagere moja huku lingine likifungwa na Okwi.

Mchezo wa kwanza Simba ilishinda mabao 4-1, kwenye Uwanja wa Taifa hivyo Simba inaingia hatua ya kwanza kwa jumla ya mabao 8-1 na sasa inasubiri mshindi wa mchezo kati ya Nkana Red Devils ya Zambia na UD Songo ya Msumbiji zinazorudiana leo mjini Lusaka.

Hata hivyo, katika mchezo wa kwanza uliochezwa Novemba 28 mwaka huu, ikiwa ugenini Nkana ilishinda mabao 2-1.

Mechi za raundi ya kwanza zitachezwa kati ya Desemba 15 na 16 na marudiano ni kati ya Desemba 27 na 28.

 

Mchezo wenyewe

Katika mchezo huo, wenyeji wakiamini Simba ingelinda ushindi wake, ilikumbana na hali ya tofauti kwamba ilicheza soka ya kujiachia kiasi cha kuwachanganya Waswazi hao.

Kocha wa Mbabane, Kinah Phiri ambaye alitamba kuiua Simba marudiano, alifanya mabadiliko ya mapema dakika ya 37 kwa kuwatoa beki, Sifiso Mabila na kumuingiza mshambuliaji Tarawallie Sallieu na dakika ya 39 akamtoa kiungo mshambuliaji Richard Mccreesh na kuingia Colani Sikhondze.

Simba ilikianza kipindi cha pili kwa kujiamini na dakika ya 54, Emmanuel Okwi aliifungia Simba bao la tatu, baada ya kuwalamba chenga wachezaji wa Mbabane kuanzia katikati ya Uwanja akiwaunga tela hadi kuujaza mpira wavuni.

Bao hilo ndilo lililowakatisha kabisa tamaa wenyeji walioonekana kuanza kulaumiana ndani na hata kwa upande wa mashabiki huku wengine wakiondoka uwanjani.

Mshambuliaji nyota kutoka Rwanda, Meddie Kagere ambaye alifunga bao la tatu mchezo wa kwanza, hakukubali kutoka uwanjani kapa bali alihitimisha karamu ya mabao alipoifungia Simba bao la nne katika dakika ya 64 kwa kuwazidi maarifa mabeki wa timu hiyo. 

MECHI ya kesho kati ya Nkana Red Devils ya Zambia na UD Songo ya Msumbiji ndio itakayoamua nani acheze na Simba hatua ya pili katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Beki wa zamani wa Simba na Yanga, Hassan Kessy anaichezea timu ya Nkana Red Devils na kama itashinda mechi dhidi ya UD Songo ya Msumbiji, itakuwa rahisi kwa Wanamsimbazi kujua siri ya wapinzani wao. Kessy amewahi kukaririwa akisema klabu yake ya Nkana Red Devils wanajua kujituma uwanjani inayotokana na wachezaji kulinda nafasi zao za kucheza. "Soka ni lile lile, ila huku mchezaji anayecheza kikosi cha kwanza anajua kulinda heshima yake, ndio maana hata mimi niliingia moja kwa moja kwenye mpango wa kocha, soka wanalichukulia kama kazi kweli kweli,"anasema.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz