Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Cannavaro aagwa, ampa mikoba Ninja

11621 Pic+canavaro TanzaniaWeb

Mon, 13 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Morogoro. Aliyekuwa nahodha wa Yanga Nadir Haroub ‘Cannavaro, amemkabidhi rasmi jezi yake Abdallah Shaibu ‘Ninja’.

Cannavaro amefikia uamuzi huo, baada ya kugoma jezi yake isitumike kwa mchezaji mwingine kama ilivyokuwa imepangwa na uongozi wa Yanga.

Cannavaro alikuwa akitumia jezi namba 23 aliyoivaa kwa miaka 12 hadi anastaafu kucheza soka na kupewa cheo cha meneja.

Baaya ya Cannavaro kumaliza kucheza jana, jezi alimkabidhi Ninja ambaye alilazimika kutoanza mchezo huo ili kumpa fursa beki huyo nguli.

Cannavaro alimkabidhi Ninja jezi hiyo ambayo sasa itakuwa inatumiwa na beki huyo ambaye nguli huyo aliliambia gazeti hili anataka beki huyo arithi kazi yake.

Nguli huyo alisema anaamini Ninja ndiye mtu anayeweza kurithi mikoba yake kwa kuwa ana amini ana uwezo mzuri wa kucheza nafasi ya beki wa kati.

Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga Hussein Nyika aliliambia gazeti hili kuwa wanajipanga kuhakikisha Cannavaro wanampeleka kusoma.

“Haya yote yatafanyika lakini hakuna kitu muhimu kama elimu kwasasa Cannavaro tumempa cheo cha umeneja tunataka kwenda kumsomesha uongozi kuhusu michezo, hata ikitokea kozi ya ukocha tunataka kuona anajifunza,”alisema Nyika.

Yanga imepiga kambi kujiandaa mashindano ya Ligi Kuu Tanzania Bara yaliyopangwa kuanza Agosti 22.

Chanzo: mwananchi.co.tz