Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CHAMA AONGOZA KUONDOKA NA TUNZO NYINGI

Image 243.png?fit=521%2C393 CHAMA AONGOZA KUONDOKA NA TUNZO NYINGI

Sat, 8 Aug 2020 Chanzo: zanzibar24.co.tz

Clatous Chama, ambae ni kiungo bora wa msimu wa 2019/20 anayekipiga ndani ya Klabu ya Simba jana kwenye kilele cha Tuzo za VPL zinazofanyika Ukumbi wa Mlimani City amesepa na tuzo binfasi mbili.

Tuzo ya kwanza ilikuwa ni ya kiungo bora baada ya kuwashinda, Lukas Kikoti wa Namungo na Mapinduzi Balama wa Yanga.

Ameibuka kuwa mchezaji bora kwa msimu wa 2019/20 akiwashinda Nicolas Wadada wa Azam FC ambaye mkononi ana tuzo ya beki bora wa msimu wa 2019/20 na beki wa Coastal Union Bakari Mwamnyeto wote wamo kwenye kikosi bora cha msimu wa 2019/20

Chama ni namba moja kwa pasi za mwisho ndani ya Simba akiwa ametoa jumla ya pasi 10 za mabao huku akifunga mabao 2 na kumfanya ahusike kwenye jumla ya mabao 12 kati ya 78 yaliyofungwa na Simba.

Chama amewashinda washindani wake ambao ni Lukas Kikoti wa Namungo mwenye pasi saba za mabao huku akitupia mabao manne pamoja na Mapinduzi Balama wa Yanga mwenye mabao matatu na pasi moja ya bao.

Chama ametupia jumla ya pasi 10 za mabao huku akifunga mabao mawili kwa msimu wa 2019/20.kiungo huyo pia amekuwa ni miongoni mwa kikosi bora cha msimu wa 2019/ 20 ambacho kilikua na wachezaji kama Aishi Manula, David Luhende, Nicolaus Wadada , Bakari Nondo, Pascal Wawa, Zawadi Mauya, Lucas Kikoti, Clatous Chama, Meddie Kagere, John Bocco, Luis Muiquissone.

Chanzo: zanzibar24.co.tz