Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CAF yawapa shavu Waamuzi Bongo

70687 CAF+pic

Sat, 10 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limewapa shavu kiaina waamuzi wanne wa Tanzania kwa kuwapangia kuchezesha pambano la Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Gor Mahia ya Kenya na Aigle Noir ya Burundi, litakalochezwa keshiokutwa mjini Bujumbura.

Waamuzi hao kutoka Tanzania waliopangwa kuchezesha mechi hiyo ya raundi ya awali ni Hery Sasii, Ferdinand Chacha, Frank Komba na Emmanuel Mwandembwa.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka CAF, Sasii ambaye ana beji ya kimataifa ya uamuzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) kama ilivyo kwa wenzake watatu, atakuwa refa wa kati kwenye mechi hiyo ambayo Aigle Noir watakuwa wenyeji.

Kwenye mechi hiyo, Frank Komba atakuwa refa msaidizi namba moja wakati Ferdinand Chacha atakuwa mwamuzi msaidizi namba mbili huku Emmanuel Mwandembwa akipangwa kama mwamuzi wa nne.

Kwa kupangwa kuchezesha mechi hiyo, waamuzi hao watakutana na nyota wawili wa Kitanzania wanaochezea Gor Mahia ambao ni mshambuliaji Dickson Ambundo na kipa David Kissu.

Ambundo amesajiliwa na Gor Mahia akitokea Alliance FC wakati Kissu amenaswa na timu hiyo ya Kenya akitokea kwenye klabu ya Singida United.

Chanzo: mwananchi.co.tz