Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CAF yaithibitisha Tanzania uwenyeji Afcon U-17

Mon, 1 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Hatimaye Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limeithibitsiha Tanzania kuwa mwenyeji wa Fainali za Kombe la Afrika kwa vijana chini ya miaka 17 (Afcon U-17) ambazo zitafanyika nchini kati ya Aprili 14-28, 2019.

Mkutano wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho hilo uliofanyika kwa siku mbili huko Sharm El Sheikh, nchini Misri umeithibitisha rasmi Tanzania kuwa wenyeji fainali hizo.

Kupitia sauti ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Serikali ya Tanzania ilimthibitishia Rais wa CAF, Ahmad Ahmad utayari wa kuwa wenyeji wa Fainali hizo na kufanya juhudi kubwa za maandalizi ya fainali hizo zitakazoshirikisha nchi nane tofauti.

Mpaka sasa, mataifa yaliyofuzu ni Angola, Cameroon, Guinea, Morocco, Nigeria, Uganda, Senegal na wenyeji Tanzania, itakayowakilisha na ‘Serengeti Boys’ iliyoshika nafasi ya tatu katika mechi za kusaka tketi ya fainali hizo za Afcon U17-2019 Kanda ya Cecafa.

Droo ya fainali hizo inatarajiwa kufanyika Desemba 20 mwaka huu, katika  michezo ya kufuzu fainali hizo, Shirikisho la soka Ulaya (UEFA) walihusika katika upande wa fedha na ufundi ambapo wataalamu wake wa ufundi walishirikiana kwa karibu na wale wa CAF.

Zoezi la kupima umri (MRI) katika michezo hiyo ya kufuzu imefanya shindano hilo kuwa na thamani zaidi.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz