Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CAF ‘yaichonganisha’ Serengeti Boys

32550 Caf+pic Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Wallace Karia

Thu, 20 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys watawafahamu wapinzani wao katika michuano ya Afcon kwa umri huo wakati Sekretarieti ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) itakapopanga ratiba ya michuano hiyo leo.

Tanzania itakuwa mwenyeji wa fainali hizo, itakayoshirikisha mataifa nane ambayo ni Uganda ambaye ni bingwa wa Cecafa, Senegal (bingwa wa Wafu Kanda A - Magharibi) na Morocco ambao ni mabingwa wa kutoka Kanda ya Kaskazini, Unaf.

Timu nyingine ni Guinea, (Bingwa wa Wafu Kanda A, Magharibi), Angola (bingwa Ukanda wa Cosafa - Kusini), Nigeria (Bingwa wa Wafu Kanda B - Magharibi) na Cameroon kutoka Kanda ya Kati Uniffac.

Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Wallace Karia akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe kuwa tayari wameshaanza kuwapokea viongozi kutoka CAF.

Karia alisema taarifa hiyo ilibidi isomwe na Waziri lakini alipata udhuru akashindwa kufika, lakini viongozi wa CAF wameanza kuwasili nchini tangu Jumanne wakikagua mambo muhimu na msingi ambayo wenyeji wanatakiwa kuyafanya.

Alisema viongozi hao kutoka CAF walikagua viwanja vya mazoezi na mechi, hoteli na hospitali azitakazotumika muda wote wa mshindano ambayo yatafanyika hapa nchini mwakani na kwa mara ya kwanza.

“Tunamba Watanzania wote katika sehemu mbalimbali wajiandae kuupokea ugeni huu kutoka CAF ili kuhakikisha mashindano haya yanafanyika hapa nchini kwani ni jambo la kihistoria kutokana haijawahi kufanyika,” alisema Karia.

Wajumbe wa CAF ambao watawasili nchini ni saba ambao ni Samson Adamu, Yasmin Hossam, Amr Ali, Mohamed Ahmed, Fayrouz Mohamed, Mohamed Alaa na Dina Mohsen.



Chanzo: mwananchi.co.tz