Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CAF kuipa makali Serengeti Boys Afcon

11337 Cuf+pic.png TanzaniaWeb

Sat, 14 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Cairo, Misri. Shirikisho la Soka Afrika (CAF), limetoa ratiba ya mechi za kufuzu fainali za Afrika.

Uamuzi huo unaonekana utasadia maandalizi ya timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’, inayojiandaa na Fainali za Afrika mwakani.

CAF jana ilitoa ratiba ya mechi za kufuzu fainali hizo ambazo Tanzania ni mwenyeji na kuijumuisha pia Serengeti Boys ingawa ina tiketi kutokana na kuwa na mwenyeji.

Katika upangaji wa makundi CAF imeweka kanda sita na kinara wa kila kanda ataungana na Tanzania.

Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa) litatoa mafunzo kwa nchi zitakazoshiriki hatua ya mtoano.

Taarifa ya Katibu Mkuu wa CAF, Amr Fahmy, ilisema uamuzi huo umepitishwa na kikao cha Kamati ya Utendaji ya shirikisho hilo kilichofanyika Julai 2017 mjini Rabat, Morocco.

Fahmy, alisema kanda hizo zinatoka Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa, Cosafa, UNAF, UNIFFAC, Wafu A na Wafu B).

“Mechi za kufuzu zitachezwa kati ya Julai na Septemba mwaka huu na timu zitajumuisha Kanda za Cosafa kituo kitakuwa Mauritius.

UNIFFAC kituo kitakuwa Equatorial Guinea, Cecafa itakuwa Tanzania, Unaf mwenyeji ni Tunisia, Wafu A mwenyeji Senegal na Wafu B ni Niger,” alisema Fahmy.

Cosafa:

Mwenyeji: Mauritius, Angola, Botswana, Lesotho, Malawi, Mauritius, Msumbiji, Namibia, Shelisheli, Afrika Kusini, Swaziland, Zambia na Zimbabwe. Kuanza: Julai 19 - 29, 2018

UNIFFAC:

Mwenyeji: Equatorial Guinea, Cameroon, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Congo, Guinea Equatorial, Gabon, DR Congo, Sao Tome na Chad. Kuanza: Agosti 3- 12, 2018

CECAFA:

Mwenyeji: Tanzania. Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda, Burundi, Sudan, Ethiopia, Sudan Kusini, Somalia na Djibouti Kuanza Agosti 11-26, 2018

UNAF:

Mwenyeji: Tunisia, Morocco, Algeria na Libya, kuanza Agosti 20-28, 2018

WAFU B:

Mwenyeji: Niger, Ivory Coast, Ghana, Nigeria, Togo, Burkina Faso, Niger na Benin. Kuanza Septemba 2- 15, 2018.

WAFU A:

Mwenyeji – Senegal, Cape Verde, Gambia, Guinea, Guinea Bissau, Liberia, Mauritania, Senegal na Sierra Leone.

Chanzo: mwananchi.co.tz