Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CAF Yaukataa Uwanja wa CCM Kirumba

Kirumba?fit=600%2C338&ssl=1 Uwanja wa CCM Kirumba

Sat, 4 Sep 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Biashara United haitaweza tena kucheza mechi zao za Kombe la Shirikisho Afrika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza kama ilivyokuwa mipango yao baada ya CAF kuukata uwanja huo na sasa wawakilishi hao watakipiga jijini Dar es Salaam.

Tayari timu hiyo ilishaweka kambi jijini Mwanza kwa wiki mbili, lakini juzi wameambiwa mechi yao ya awali dhidi ya FC Dikhil ya Djibouti itapigwa Benjamin Mkapa, kwa vile Kirumba imeshindwa kukidhi vigezo vilivyotakiwa.

Meneja na mratibu wa Biashara amesema wamelazimika kubadili kila kitu kwani walikuwa Kirumba kwa zaidi ya siku 10 na wachezaji walikuwa wamezoea mazingira hayo hivyo wapo kwenye hatua za mwisho za kuhamishia kambi Dar ili kuanza upya maandalizi.

Chanzo: globalpublishers.co.tz