Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bushiri aingia matatani Mbao FC

38355 Bushri+pic Bushiri aingia matatani Mbao FC

Fri, 25 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Mshambuliaji wa Mbao FC, Said Khamisi amemtaja kocha mpya Ali Bushiri ndio chanzo cha kushindwa kufunga mabao katika Ligi Kuu Tanzania Bara.

Akizungumza jana, Khamisi alisema kitendo cha kubadilishwa namba na Bushiri kimemuondoa katika nafasi yake nzuri ya kufunga mabao.

Alisema kabla ya ujio wa Bushiri, alikuwa akicheza nafasi ya mshambuliaji wa kati iliyompa fursa ya kufunga mabao tofauti na sasa anakocheza pembeni.

Kinda huyo aliyeanza kwa kasi Ligi Kuu kwa kufunga mabao sita alipokuwa chini ya kocha Amri Said ‘Stam’, hajafunga bao tangu Bushiri alipotwaa mikoba.

Mara ya mwisho kufunga bao ilikuwa mechi dhidi ya Mwadui FC timu hiyo ikiwa chini ya Stam katika mchezo walioshinda mabao 2-1 dhidi ya Biashara United Desemba 17, mwaka jana.

Bushiri anampanga mchezaji huyo kucheza winga wa kulia na namba yake amepewa Rajesh Kotecha na Evarigestus Mujwahuki.

Khamisi alisema anatarajia kuzungumza Bushiri ili kumrudisha katika nafasi ya mshambuliaji aliyokuwa akipata fursa ya kufunga mabao.

“Kasi yangu ya ufungaji mabao imepungua, lakini si kwamba kiwango ndicho tatizo, tuna kocha mpya nimebadilishwa majukumu ingawa napambana nirudishwe katika nafasi ya mwanzo,”alisema Khamisi.

Kinda huyo alisema kabla hajaanza kucheza soka la ushindani alikuwa akicheza namba 10 iliyompa fursa kufunga mabao.



Chanzo: mwananchi.co.tz