Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bolt aanza mazoezi ya soka nchini South Africa

Wed, 31 Jan 2018 Chanzo: bongo5.com

Mstaafu wa mbio za sprinter kutoka nchini Jamaika Usain Bolt amekuwa akifanya mazoezi na timu inayoshikilia uskani katika ligi ya Absa Premiership ya nchini South Africa ambao ni Mamelodi Sundowns.



Licha ya kuwa mwanariadha mwenye kasi katika mbio za mita 100 na 200, Bolt amekuwa akivutiwa sana na soka na mara nyingi amekuwa akiwaambia vyombo vya habari kuwa atachezea mchezo huo baada ya kustaafu michezo ya mbio.



Imethibitishwa kwamba Bolt mwenye umri wa miaka 31 atafanya majaribio na timu ya ligi ya Bundesliga Borussia Dortmund mwezi Machi.

“Dortmund walisema kwamba mwaliko daima umefunguliwa, hivyo basi ni mimi tu kutibu majeruha yangu na kupata uwezo wa kucheza soka” Bolt alinukuliwa na The Sun mwaka jana Novemba.

Kampuni ya michezo Puma, ambaye ina muidhinisha Bolt na kudhamini timu hiyo Mamelodi Sundowns wali muanzishia mafunzo ya soka Bolt Jumatatu asubuhi huko Chloorkop ambayo ni sehemu inayotumika na Mamelodi Soundowns kufanya mazoezi.



Mkutano wa waandishi wa habari ulifanyika baada ya Bolt kufanya mazoezi na alifafanua kwamba matakwa yake ni siku moja kucheza mchezo huo lakini pia alikiri kwamba anahitaji kufanya kazi kubwa ili aweze kupata uzoefu kabla ya kurejea nchini Jamaica.

Chanzo: bongo5.com