Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bodi ya Ligi yafungia viwanja vitatu kutumika Ligi Kuu Bara

71482 Viwanja+picha

Thu, 15 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Bodi ya Ligi limevifungia viwanja vitatu uwanja wa Mwadui, Manungu na Mabatini kutumika katika msimu huu wa Ligi Kuu Bara hadi hapo vitakapofanyiwa marekebisho.

Akizungumza Dar es Salaam, Afisa mtendaji mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura alisema viwanja vilivyofungiwa ni pamoja na uwanja wa Mwadui, Manungu na Mabatini.

Alisema sababu za kufungia viwanja hivyo ni kubainika uzio wake unamapungufu ni hatari kwa wanasoka wenyewe kwa mfano uwanja wa Manungu, Mabatini  vyote vimezungushiwa mabati wakati Mwadui imezungushiwa makuti.

"Ukaguzi wa viwanja unaendelea na tayari tumesha fungia viwanja vitatu kwa sababu zilizotajwa na tumeshawatengea viwanja watakavyotumia msimu ujao na kuwa viwanja vyao vya nyumbani," alisema na kuongeza kuwa.

"Mtibwa watatumia uwanja wa Jamhuri, Ruvu Shooting watatumia Isamuyo na Mwadui watatumia Kambarage watarudi kwenye viwanja vyao hadi hapo watakapomaliza ukarabati," alisema Wambura.

Chanzo: mwananchi.co.tz