Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bodi ya Ligi TPLB yaiadhibu Yanga

NGAYAZIII Bodi ya Ligi TPLB yaiadhibu Yanga

Thu, 8 Jul 2021 Chanzo: eatv.tv

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Julai 6,2021 ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi Kuu na kufanya maamuzi yafuatayo.

Submitted by George David on Alhamisi , 8th Jul , 2021 Kiungo machachari wa Yanga, Fiesal Salum akimtoka Erasto Nyoni wa Simba katika Dabi ya Kariakoo iliyopigwa Julai 3 mwaka huu kwenye Dimba la Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam.

Mechi Namba 208;Simba 0-1

Yanga Timu ya Yanga imetozwa faini ya Sh.3,000,000 (Milioni tatu) kwa makosa yafuatayo.

-kutumia mageti ya uwanja wa Uhuru kuingia uwanja wa Benjamin Mkapa badala ya mlango maalum unaotumiwa na timu.

-Kutumia mageti ya uwanja wa Uhuru kuingia uwanja wa Benjamin Mkapa badala ya mlango maalum unaotumiwa na timu. -Kutumia mlango wa chumba cha waandishi wa habari badala ya mlango maalum unaotumiwa na timu.

-Kuingia uwanjani kupasha misuli kwa kutumia mlango(Gate B) ambao haukupangwa kutumika kwa namna yoyote.

-Kutumia chumba cha wafanya usafi wa uwanja kwa ajili ya kubadilisha nguo badala ya chumba maalum cha kubadilishia nguo. Pia timu ya Yanga inatakiwa kulipa Tsh.850,000/= ikiwa n gharama ya ukarabati wa mageti yaliyovunjwa wakati wa kuingia uwanjani pamoja na makufuli ya uwanja wa Benjamin Mkapa yaliyoharibiwa katika tukio.

Matukio hayo yalitokea katika mchezo uliochezwa Julai 3,2021 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam. Adhabu hii imetolewa kwa kuzingatia kanuni ya 15(15) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za mchezo.

-Mechi Namba 287;Ruvu Shooting Fc 1-1 Polisi Tanzania Fc

Timu ya Ruvu Shooting Fc imepewa onyo kali kwa kosa la mchezaji wa timu hiyo Saamson Kwakwala kuvaa jezi namba 71 mgongoni.

Kamati inazikumbusha Klabu zote kuwa na namba zinazoruhusiwa ni kati ya namba 1(Moja) hadi 60(Sitini ) tu.

Tukio hilo lilitokea katika mchezo uliochezwa Juni 24, 2021 kwenye uwanja wa Mabatini mkoani Pwani.

Adhabu hii imetolewa kwa kuzingatia kanuni ya 15(2.5) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.

Chanzo: eatv.tv