Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bodi ya Ligi , TFF kuamua tarehe mpya mechi ya Simba na Yanga

Yanga  Ed Bodi ya Ligi , TFF kuamua tarehe mpya mechi ya Simba na Yanga

Tue, 11 May 2021 Chanzo: ippmedia.com

Bashungwa ametoa agizo hilo katika kikao cha pamoja kilichofanyika kati ya wizara hiyo, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Bodi ya Ligi, Baraza la Michezo Tanzania na klabu za Simba na Yanga.

Mchezo huo namba 208 wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliokuwa uchezwe Jumamosi Mei 8 mwaka huu uliahirishwa kutokana na mkanganyiko uliozuka baada ya mchezo huo kusogezwa mbele kutoka saa 11:00 jioni hadi saa 1:00 jioni.

Aidha, waziri ameahidi kuitisha kikao cha pamoja ili kuondoa jakamoyo lililopo kutokana na kuwepo kutokuaminiana kati ya TFF na baadhi ya vilabu nchini, hasa klabu ya Yanga.

Pia, ametumia nafasi hiyo kuwaomba radhi mashabiki na wapenzi wa soka nchini kufuatia kusogezwa mbele kwa saa kadhaa na baadaye kuahirishwa kwa mchezo huo uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu

Chanzo: ippmedia.com