Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bocco, mtambo wa mabao Simba uliowajibu mashabiki kwa vitendo

49824 BOCCO+PIC

Mon, 1 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mmoja wa wachezaji nyota anayetamba katika Ligi Kuu Tanzania Bara aliyewahi kupitia kipindi kigumu ni nahodha wa Simba John Bocco.

Mshambuliaji huyo mrefu amewahi kupata wakati mgumu kwa mashabiki wakidai amekuwa akikosa mabao katika mechi za Simba licha ya kupata nafasi nzuri akiwa ndani ya eneo la hatari.

Baadhi ya mashabiki wanamuona ni mchezaji wa kawaida asiyekuwa na madhara, lakini kumbe ni nyota muhimu katika kikosi cha Simba na Taifa Stars.

Ingawa mara kadhaa amewahi kubezwa, Bocco amekuwa akiwajibu wabaya wake kwa vitendo uwanjani hasa katika mechi muhimu za kuamua matokeo.

Bocco ambaye alicheza Azam kwa miaka 10, alisajiliwa Simba mwaka 2017 na msimu huu ameifungia timu hiyo mabao tisa kwenye Ligi Kuu na kutoa pasi nne za mabao. Pia amefunga mabao matatu katika Ligi ya Mabingwa Afrika na kutoa pasi mbili za mabao.

Bocco alifunga mabao mawili akichangia ushindi wa Simba wa mabao 4-1 dhidi ya Mbabane Swallos ya Swaziland iliyofanyika Dar es Salaam, pia alifunga bao Simba ilipopata kipigo ugenini cha mabao 2-1 dhidi ya Nkana Red Devil ya Zambia.

Bocco alitoa pasi ya bao lililofungwa na Meddie Kagere katika ushindi 1-0 iliyopata Simba dhidi ya Al Ahly ya Misri, alitoa pasi nyingine muhimu ya bao la ushindi lililofungwa na Clatous Chama Simba iliposhinda mabao 2-1 dhidi ya AS Vita ya DR Congo na kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ligi Kuu Bara

Bocco amefunga mabao tisa kwenye Ligi Kuu msimu huu, matatu akifunga kwa kichwa, matatu kwa mguu na matatu kwa penalti huku akitoa pasi nne za mabao.

Mshambuliaji huyo alifunga mabao mawili Simba ilipoichapa Mwadui mabao 3-1 kwenye Uwanja wa Kambarage Shinyanga pia alifunga bao moja Simba iliposhinda mabao 3-0 dhidi ya Singida United.

Alifunga tena bao moja na kuisaida timu yake kupata ushidni wa mabao 3-0 dhidi ya Mwadui katika mchezo wa mzunguko wa pili. Nguli huyo alifunga mabao mawili Simba ilipoichapa African Lyon 3-0, alifunga bao moja ilipoifunga Azam mabao 3-1 kabla ya kuweka kambani mawili na kuingoza timu yake kuichapa Stand United 2-0.

Pasi za Mabao

Bocco alitoa pasi ya bao lililofungwa na Kagere Simba ilipoifunga Prisons bao 1-0, pia alitoa pasi ya bao la tatu lililofungwa na Emanuel Okwi Simba ilipoitandika Alliance mabao 5-1, alitoa tena pasi ya bao la pili lililofungwa na Muzamir Yassin Simba ilipoifunga Mwadui mabao 3-0 na katoa tena pasi muhimu ya bao lililofungwa na Kagere, Simba ilipoibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya watani wao wa jadi Yanga.

Katika mashindano ya msimu huu, huwezi kutaja mafanikio ya Bocco bila kumtaja Meddie Kagere na Emmanuel Okwi raia wa kigeni anaocheza nao pacha katika safu ya ushambuliaji chini ya Kocha Mbelgiji Patrick Aussems.

Kadi nyekundu

Mchezaji huyo msimu huu ameonyeshwa kadi nyekundu mara moja katika mchezo uliofanyika Septemba 23, mwaka jana dhidi ya Mwadui ugenini uliomalizika kwa Simba kushinda mabao 3-1.

Bocco alionyeshwa kadi hiyo baada ya kumchezea madhambi Revocutus Mgunga walipokuwa wakiwania mpira.

Kadi hiyo ilisababisha Bocco akose michezo mitatu ya mzunguko wa kwanza dhidi ya Yanga African Lyon na Stand United.

Msolla afunguka

Kocha Mshindo Msolla anasema Bocco amebadilika sana kiuchezaji na amekuwa mfano mkubwa kwa wenzake.

“Katika siku za karibuni kuanzia mechi ya kimataifa na AS Vita ya Congo, Bocco alinishangaza kiwango chake kiwango chake cha kujitolea kimekuwa cha juu.

“Ameonyesha dhamira ya kujituma si Bocco wa zamani. Ushauri wangu kwake haya aliyoamua kufanya ayaendeleze kwa sababu naamini Bocco ni mtu anayependa mazoezi na mchango wake ni mkubwa.

“Ukiangalia amecheza Ligi Kuu kwa miaka 10 Azam kwa umri wake na kiwango alichonacho anaonekana ni mtu wa mazoezi na kujituma ni mfano kwa wenzake,”anasema Msolla.

Kocha wa zamani wa Yanga Kennedy Mwaisabula anasema Bocco ni mshambuliaji, lakini awali hakuwa akijitambua.

“Ni mmoja kati ya washambuliaji wazuri nchini nafikiri sasa amejitambua. Ana tatizo moja kubwa anakosa mabao lakini ameshajua tatizo lake hivyo anatengeneza nafasi ameona hiyo ndio silaha yake kubwa.

Mwaisabula ambaye pia amewahi kuinoa Cargo, anasema Bocco ni mchezaji ambaye amekuwa chachu ya mafanikio katika kikosi cha Simba na Taifa Stars.



Chanzo: mwananchi.co.tz