Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bocco apewa program ya kipekee Uturuki

9380 Pic+bocco TanzaniaWeb

Thu, 2 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kartepe. Mshambuliaji na nahodha wa kikosi hicho, John Bocco ' Adebayo' amepewa programu ya mazoezi ya peke yake ili kumweka fiti.

Bocco ambaye ni mchezaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita, amekuwa akifanya mazoezi ya kukimbia na kunyoosha misuli akitumia vifaa maalumu.

Program hiyo imeanza jana Ijumaa na ameendelea nayo kwa siku ya leo Jumamosi.

Daktari wa Simba, Yassin Gembe amesema, hiyo ni program maalumu kwa siku hizo na si majeruhi bali ana maumivu kidogo.

" Anafanya programu hiyo kwa ajili ya kumjenga lakini ifahamike kuwa si majeruhi ila ana maumivu kidogo,"alisema Gembe.

Chanzo: mwananchi.co.tz