Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bocco apewa kitambaa Stars

68401 Pic+bocco

Sun, 28 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

BENCHI la Ufundi la timu ya Taifa Tanzania 'Taifa Stars' limemteua mshambuliaji John Bocco kuwa nahodha wa timu hiyo kuelekea mchezo dhidi ya Kenya.

Stars itacheza michezo ya kufuzu CHAN dhidi ya Kenya 'Harambee Stars'  Julai 28 jijini Dar es Salaam huku marudiano yakiwa Agosti 4 jijini Nairobi, Kenya.

Nafasi ya nahodha Stars ilikuwa ikishikiliwa na Mbwana Samatta lakini mashindano haya yanamfanya asiwepo kutokana na kushirikisha wachezaji wanaocheza ligi za ndani.

Licha ya uteuzi huo, Bocco atakuwa akisaidiana na Juma Kaseja, Kelvin Yondani na Erasto Nyoni ambao wote waliwahi kuwa manahodha katika klabu zao.

Aliyewahi kuwa kocha wa Yanga na mchambuzi wa soka, Kenny Mwaisabula alisema suala la uteuzi wa nahodha katika timu haliangalii ufundi zaidi ya mtu sahihi ambaye ataweka mawasiliano mazuri baina ya benchi la ufundi na wachezaji.

"Ni suala la benchi la ufundi kuangalia yupi ambaye ni sahihi kuwa kiunganishia na ana mawasiliano mazuri na wenzake," alisema.

Pia Soma

Licha ya kupewa unahodha Stars, Bocco pia ni nahodha wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba.

Chanzo: mwananchi.co.tz