Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Boban ampagawisha mzungu Lyon

16112 Pic+boban TanzaniaWeb

Fri, 7 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kocha wa African Lyon, Soccoia Lionel ameshangazwa na kiwango anachokionyesha kiungo mshambuliaji, Haruna Moshi ‘Boban’ akidai anastahili kucheza nje ya nchi.

Boban alionekana akijituma uwanjani huku Lionel akionekana kushangazwa na kiwango cha kiungo huyo wa zamani wa Simba na Taifa Stars.

“Ni mchezaji mwenye vitu vikubwa kwenye mguu wake, kwanza hana mzaha wakati wa mazoezi, kifupi anajitambua ni nani anapokuwepo uwanjani, nafurahishwa sana na uchezaji wake,”alisema Lionel.

Kocha huyo alisema anaamini Boban atakuwa chachu ya mafanikio ndani ya kikosi chake katika safu ya ushambuliaji anakocheza pacha na Victor Da Coasta raia wa Ufaransa.

Boban alisema amepania kucheza kwa kiwango bora msimu huu na kurejesha heshima ya African Lyon ambayo imerejea Ligi Kuu.

“Kikubwa tutakachofanya ni kuhakikisha tunajituma katika mechi zote ili kufikia malengo ambayo ni siri yetu, lakini pia waamuzi wajaribu kufanya kazi zao kwa usahihi ili kuruhusu vipaji vya wachezaji kuonekana.

“Haipendezi waamuzi kupigiwa kelele za kutokuwa sawa miaka nenda rudi, hiki si kitu kizuri kwao soka inatakiwa kusonga mbele na siyo vinginevyo,”alisema Boban ambaye sio mzungumzaji sana na vyombo vya habari.

African Lyon ni miongoni mwa timu sita zilizopanda daraja ikiungana na Coastal Union, JKT Tanzania, KMC, Alliance na Biashara United.

Chanzo: mwananchi.co.tz