Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bingwa mtetezi akacha riadha Taifa

Riadha2 Data Washirki wa Riadha Taifa

Fri, 8 Oct 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Mkoa wa Pwani umeshindwa kusafirisha timu kwenda Arusha kwa ajili ya mashindano ya riadha ya taifa kwa kile ilichoelezwa ni kukosa pesa ya usafiri kwa wanariadha wao 15.

Timu hiyo ambayo iliweka kambi kwenye kituo cha michezo cha Filbert Bayi, Kibaha kwa siku kadhaa kwa ajili ya maandalizi ya mashindano hayo yaliyofunguliwa leo kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Akifichua chanzo cha mkoa kushindwa kusafirisha timu, Bayi mwanariadha nyota wa zamani aliyewahi kuvunja rekodi ya dunia ya mbio za mita 1500 alisema uongozi ulidai haina pesa za usafiri kutoka Pwani kwenda Arusha.

Mwenyekiti wa Riadha Pwani, Joseph Luhende ambaye yuko Arusha kwenye mashindano hayo alisema mkoa ulipata changamoto katika kusafirisha timu, lakini walizikamilisha.

"Nani amekwambia hatujaleta timu? Mbona tupo," amehoji Luhende bila kufafanua uwepo wa timu hiyo kwenye mashindano hayo huku Bayi akifichua kwamba, wanariadha hao wamesafirishwa na Taasisi ya FBF na si mkoa.

"Walitangaza kutoa timu kwenye mashindano kwa kukosa nauli, lakini kwa kuwa wanariadha wengi wanatokea kwenye kituo cha FBF, nikasema hapana, mimi wanariadha wangu nitawasafirisha wenyewe.

"Niliwambia haiwezekani vijana wamefanya mazoezi mwaka mzima bila kufanya mashindano na mkoa ushindwe kutoa gharama za usafiri pekee kwenye mashindano haya, FBF ikalazimika kuwasafirisha wanariadha 17 na makocha watatu," amesema.

Amedai mkoa wa Pwani umeshindwa kuwajibika kwa timu yao kuanzia kwenye maandalizi ya kambi na kusafirisha timu, jambo ambalo linapoteza afya ya ushindani wa mkoa huo ambao ni mabingwa watetezi.

"Bora viongozi wa riadha  Pwani wajiuzulu, kama wanashindwa kupeleka timu kwenye mashindano ya taifa, wajibu wao katika mkoa ni nini," alihoji Bayi.

Ingawa Luhende amesema changamoto zote ambazo timu yao imepitia ni kutokana na kukosa sapoti ya wadau wa mkoa wa Pwani.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz